loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kampeni kupinga rushwa ya ngono inavyozaa matunda

TAASISI ya kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru), ilianzisha klabu za kampeni katika vyuo na shule mbalimbali nchini za kupinga vitendo vya rushwa ya ngono na kuwapa mafunzo jinsi ya kutoa taarifa wakutanapi na vitendo hivyo vya unyanyasaji.

Katika mafunzo hayo, vyuo mbalimbali nchini vimefikiwa na elimu hiyo iliyotolewa na maafisa kutoka Takukuru wakishirikiana na wanaharakati wengine wa kupambana na vitendo viovu ambapo walengwa katika mafunzo hayo walizungumzia hali ilivyo na kusema bado rushwa hiyo ipo na ima madhara makubwa kiuchumi,kijamii na kiutamadini.

Madhara makubwa yatokanayo na rushwa ya ngono vyuoni na shuleni ni kuporomoka kwa elimu na kuporomoka kwa sifa ya taaluma ya vyuo vikuu na Elimu ya juu.

Katika vyuo, madhara yanayosababishwa na rushwa ya ngono ni kuanguka kwa elimu na maadili, kupatikana kwa wasomi wenye uwezo duni wasiokuwa na sifa stahiki, wasomi kupata vyeti wasivyostahili.

Kadhalika kwa elimu ya shule za msingi na sekondari, ni wanafunzi kukatiza masomo kwa sababu ya mimba, utoro, maadili kuporomoka.

Athari nyingine ni kuajiriwa watu wasiokuwa na sifa na utendaji kazi kuanguka makazini, mahusiano mabaya makazini, kuongezeka kwa magonjwa ya zinaa na Ukimwi, ongezeko la mimba zisizotarajiwa, ukiukwaji wa haki za binadamu na utawala bora.

Sasa basi kupitia Takukuru, ilianzisha klabu za wapinga rushwa shuleni na vyuoni kupitia mafunzo ya kampeni ya ‘’Vunja ukimya kataa rushwa ya ngono’’.Kampeni ambayo inazaa matunda bora kila uchwao kutokana na wahalifu kutiwa mbaroni.

Hivi karibuni mkoani Mbeya, Singida na Mwanza Takukuru imewakamata watuhumiwa mbalimbali wa makosa ya rushwa ya ngono wakiwemo wanafunzi ambao walipewa mafunzo hayo na kusaidia kufanikisha kukamatwa kwao.

Katika tukio moja mkoani Mbeya, Mwalimu Mkuu wa shule moja ya msingi anashikiliwa na Takukuru baada ya kuwekewa mtego akiwa nyumba ya kulala wageni na mwanafunzi wake wa darasa la saba.

ZIMEBAKI siku nne kufi kia siku ya Uchaguzi Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi