loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Dk Abassi: Tuko makini kuwekeza kwenye maendeleo

KATIBU Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Hassan Abbasi amesema Tanzania ipo makini kuwekeza kwenye mambo ambayo ni muhimu katika kuleta maendeleo ya watu kama ilivyo kwa ujenzi wa Reli ya ya Kisasa (SGR) itakayorahisisha usafi ri wa abiria na mizigo.

Abbasi ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, alisema kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro itachukua muda mfupi hatua itakayopunguza muda mwingi unaopotea barabarani na kufanya wananchi kuwahi kufanya kazi nyingine za maendeleo.

Alisema hayo jana Ihumwa jijini Dodoma wakati akizungumza na menejimenti ya wizara yake yenye dhamana kuisemea serikali kupitia Idara ya Habari (Maelezo) iliyotembelea mradi wa SGR kujionea maendeleo yake .

“Wizara ya habari ni wizara muhimu sana katika nchi yetu na mradi huu pia. Ndiyo wizara yenye dhamana na habari kwa maana hiyo tumekuwa tukiutangaza sana na kuulinda mradi huu ili kuwaonesha watanzania nini kinaendelea kwenye huu mradi,” alisema Abbasi.

Akisisitiza namna nchi ilivyo makini kuwekeza kwenye mambo ambayo ni muhimu katika kuleta manufaa na maendeleo ya watu, Dk Abbasi alisema ni utamaduni mpya kwenye nchi kuwa na taifa la wachapakazi, wanaojiamini na wanaopenda mambo mazuri yanayoletwa na serikali kwa manufaa ya wananchi wake.

“Tunaposema huu ujenzi wa reli ni kitu, ndiyo ni kitu, reli ya SGR ni kitu kinachokwenda kuleta maendeleo ya watu. Utakapoweza kusafiri kwa saa tatu au dakika 90 Dar es Salaam hadi Morogoro umepunguza muda mwingi wa kupoteza barabarani na kuwahi kwenda kufanya kazi,” alisema.

SGR ni miongoni mwa miradi mikubwa inayotekelezwa ambao serikali imewekeza takribani Sh trilioni saba kwa kipande cha Dar es Salaam, Morogoro hadi Mkutupora mkoani Singida.

Kipande cha Morogoro hadi Dodoma kimefikia asilimia 42 hadi kukamilika kwake.

Akitoa maelezo ya mradi huo kwa mwajumbe wa menejimenti ya wizara hiyo, Meneja wa mradi kipande cha Morogoro hadi Makutupora mkoani Singida, Mteshi Tito alisema reli hiyo itatumiwa na treni ya abiria itakayokuwa na mwendo wa kasi ya kilometa 160 kwa saa.

WASIMAMIZI wa vituo na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi,wameonywa kujiepusha na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Morogoro

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi