loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Shibuda: Vyama kutishia kuungana ni uchokozi

BARAZA la Vyama vya Siasa nchini limezungumzia kitendo cha chama cha ACT –Wazalendo kuamua kumpigia debe mgombea wa chama kingine na kusema kilichofanyika ni uchokozi wa siasa.

Mwenyekiti wa baraza hilo, John Shibuda alisema hayo juzi kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam ambao pamoja na masuala mengine, alikemea wagombea wanaochochea vurugu katika kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 28 mwaka huu.

“Yanayozungumzwa ni uchokozi wa siasa kwa sababu vyama vyote vinaelewa sheria na kanuni zinavyosema. Hata kunishirikisha hawakunishirikisha,” alisema mwenyekiti huyo.

Shibuda alisema hayo baada ya mwandishi wa gazeti hili kutaka kufahamu kauli ya baraza kuhusu baadhi ya vyama vya siasa kusitisha kampeni ikiwamo ACT Wazalendo ambacho mgombea wake wa urais, Bernard Membe kutoendelea na kampeni na badala yake, chama kinampigia debe mgombea wa Chadema, Tundu Lissu.

Kwa mujibu wa taarifa za chama, Membe ambaye haendelei na kampeni, kabla ya kusimama alifanya mikutano jimbo la Lindi mjini, Kilwa Kaskazini katika eneo la Njinjo na mkoani Pwani ambako alihutubia katika eneo la Ikwiriri, jimbo la Rufiji.

Baada ya mgombea wa ACTWazalendo Zanzibar, Maalimu Seif Sharif kukaririwa akimuombea kura mgombea urais wa Chadema, Tundu Lissu na kisha kiongozi wa chama hicho, Kabwe Zitto akitamba kuwa watasimamisha mgombea mmoja bara, ofisi ya Msajili wa Vyama ilikiandikia chama hicho barua.

Kutokana na vuguvugu hilo, Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza alivionya vyama vya siasa nchini vyenye nia ya kuanzisha ushirikiano wa kusimamisha mgombea mmoja katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu akisema vitakuwa vinajitafutia adhabu.

WASIMAMIZI wa vituo na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi,wameonywa kujiepusha na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi