loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wachezaji Arsenal wapewa ubalozi wa kitalii Rwanda

NAHODHA wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang ameitwa mtoto wa sokwe Igitego katika harakati za kukuza utalii wa wanyama hao nchini Rwanda. Jina hilo lina maana ya mabao kwa lengo la kukusanya uhifadhi wa wanyamapori, alisema Aubameyang.

Mwenzake, Hector Bellerin, aliitwa Iriza, akimaanisha mzaliwa wa kwanza, wakati kipa Bernd Leno aliitwa Myugariro wakimaanisha beki. Klabu hiyo ilisaini mkataba wa udhamini wa miaka mitatu wa pauni milioni 30 Mei 2018 na wakala wa utalii wa Rwanda.

Sokwe 24 (wa kike tisa na wa kiume 15) walipewa majina Alhamisi iliyopita na walinzi wa hifadhi, madaktari wa wanyama, waongoza watalii na wachezaji watatu wa Arsenal.

Mmoja wao aliitwa Amabwiriza lenye maana ya mwongozo kama wito kwa wageni kufuata miongozo ya corona.

Majina mengine waliyopewa watoto wa sokwe yalikuwa Amarembo lenye maana ya lango, Nkomezamihigo maana yake endelea nayo, Kazeneza - karibu, Umuyobozi - kiongozi na Umuganga - daktari wa wanyama.

Takribani sokwe 300 wamepewa majina tangu 2005 katika juhudi za kufuatilia maisha yao na kuwalinda dhidi ya majangil

VIGOGO wawili wa soka nchini Hispania Barcelona na Real ...

foto
Mwandishi: KIGALI, Rwanda

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi