loader
Wilder, Klopp waitaka EFL kuokoa timu nje ya EPL

Wilder, Klopp waitaka EFL kuokoa timu nje ya EPL

KOCHA wa Sheffi eld United, Chris Wilder amesema klabu ziko wazi kutoa msaada wa fedha kwa klabu ambazo hazipo Ligi Kuu. Suala hilo limekuja la haraka baada ya uamuzi wa serikali kuzuia mashabiki kuingia viwanjani tangu mwanzo wa mwezi Oktoba.

Uamuzi huo ulifanywa kufuatia kuongezeka la wagonjwa wa corona. “Itaamuliwa na klabu za Ligi Kuu,” alisema Wilder, kocha wa Blades tangu 2016. “Ikiwa chochote kinaweza kufanywa na Ligi Kuu na wanafanya uamuzi kwa pamoja kusaidia basi tutafanya hivyo,”.

Ligi Kuu inasubiri mapendekezo kutoka kwa Shirikisho la Soka kuhusu ombi la kununuliwa la pauni milioni 250. Wilder aliongeza:

“Ninawahurumia klabu nje ya Ligi Kuu kwa sababu wanategemea mashabiki wanaokuja viwanjani”.

“Kutoka kwenye mtazamo wa biashara wamepata hasara kubwa na tunatumani kila mtu atapitia, lakini lazima kuwe na wasiwasi juu ya kile kinachoendelea kwa sasa.

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp ameongeza kuwa “mpira wa miguu unapaswa kujaribu kujisaidia sisi na wenyewe”.

“Kwa jumla nadhani watu walio katika nafasi nzuri wanapaswa kuwasaidia watu walio katika nafasi ambayo si nzuri,” alisema Mjerumani huyo.

“Lakini msimamo wa klabu zote kwa sasa sio rahisi sana, sote tunajua.”

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/332490dba8ce82fd2c7715cc99b78403.jpg

CHAMA cha Makocha wa Ligi Kuu England ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi