loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Amri Said kufumua kikosi chake

BAADA ya Mbeya City kupoteza mchezo wa nne mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kocha Amri Said ameshindwa kuvumilia na ametangaza kufanya maamuzi magumu ya kufumua kikosi chake.

Mbeya City ilipata kipigo cha bao 1-0 juzi dhidi ya Namungo katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya, matokeo yanayozidi kuwabakiza mkiani na kuwapa presha kubwa.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Said alisema inabidi afumue safu yake ya ushambuliaji na kuwaondoa vijana aliowaamini na kuwapa wale waliokuwepo tangu msimu uliopita ili kupata matokeo mazuri.

“Tunatengeneza nafasi nyingi ila vijana wangu wanakosa utulivu katika umaliziaji. Pia hata safu ya ulinzi wamekuwa wakifanya makosa yanayotugharimu hivyomni lazima nifanye mabadiliko,” alisema.

Kocha huyo wa zamani wa Biashara United alisema walifanya usajili wa vijana wengi ila atawaweka kwanza pembeni wajifunze kwa wengine ili wasirudie makosa.

Alisema kila mchezo wanabadilika baada ya kufanyia kazi mapungufu yao lakini matatizo yale yale yanajirudia. Said alisema anaamini akifanya mabadiliko watapata matokeo mazuri kuanzia michezo ijayo ambapo wanatarajiwa kukutana na Tanzania Prisons.

Kwa upande wa Kocha wa Namungo FC, Hitimana Thiery alisema amefurahi kupata ushindi huo kwani wachezaji wake walipambana kwa moyo wa kujitolea.

Alisema mchezo huo licha ya kuwa mgumu, wachezaji wake walicheza kwa ari. Thiery alisema ligi imekuwa ni ngumu ila anaamini kadiri wanavyosogea kikosi chake kinaanza kuelewana na baadaye kitabadilika na kufanya vizuri zaidi.

Matokeo hayo yanaifanya Mbeya City kuendelea kushika mkia bila pointi wala bao la kufunga katika michezo minne huku Namungo ikifikisha pointi sita na kuwa katika nafasi ya saba kabla ya michezo ya jana.

WASIMAMIZI wa vituo na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi,wameonywa kujiepusha na ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi