loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Yanga, Mtibwa kazi ipo

YANGA leo watakuwa ugenini kucheza dhidi ya wakata miwa wa Manungu, Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Yanga imekuwa mtumwa wa Mtibwa baada ya kushindwa kufurukuta katika uwanja huo tangu msimu wa 2018/2019 ambapo imeadhibiwa mara tatu kabla ya mwaka huu kukutana katika Kombe la Mapinduzi, Zanzibar na kutoka sare ya bao 1-1.

Unaweza kuwa mchezo mgumu hasa kwa Yanga ambao wanakutana na uwanja ambao sio mzuri sana lakini pengine utakuwa kipimo kwa wachezaji wapya ambao baadhi wameshindwa kung’ara katika viwanja vizuri.

Yanga ina pointi saba ilizovuna katika michezo mitatu iliyopita ikishinda miwili na kupata sare moja na Mtibwa imecheza michezo mitatu imepata sare mbili na kushinda mmoja na kufikisha pointi tano.

Safu ya ushambuliaji ya Yanga inayoongozwa na Michael Sarpong, Waziri Junior, Yacouba Songne, Ditram Nchimbi bado haijaonesha makali yake ipasavyo ingawa safu ya ulinzi na kiungo iko vizuri.

Lakini kocha Zlatko Krmpotic huenda akaja na mbinu mpya za kuwafunga Mtibwa baada ya kusema amepokea maoni ya wadau waliokuwa wanalalamikia mfumo wake kutowapa nafasi washambuliaji kufunga.

Beki Shomari Kibwana atakutana na timu yake ya zamani Mtibwa kwa mara ya kwanza tangu alipojiunga na Yanga msimu huu.

Aidha, Mtibwa Sugar sio timu ya kubeza kwani ina kikosi kizuri ilichosajili msimu huu lakini pia ina wachezaji wazoefu kama Jaffar Kibaya, Hassan Kessy, Haruna Chanongo na wengine ambao wanaweza kuibeba timu.

Kocha wake Zuberi Katwila hataki kurudia makosa ya msimu uliopita, amekuwa akijitahidi apate matokeo mazuri ili kutoingia kwenye presha mwishoni mwa ligi.

Michezo mingine itakayochezwa leo ni Ruvu Shooting dhidi ya Biashara na Mwadui dhidi ya Ihefu. Timu zote zinahitaji matokeo mazuri kutoka walipo na kuingia nafasi nyingine itakayowaweka salama.

KIKOSI cha Yanga chini ya kocha mpya Cedric Kaze kimeendelea ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi