loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

AZAM, POLISI ZATAKATA

AZAM FC imepanda kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons, mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga, Rukwa jana.

Bao hilo lilifungwa dakika ya 89 kwa kichwa na mshambuliaji Prince Dube(pichani) baada ya kupata mpira wa kona uliopigwa na Idd Nado.

Huo ni ushindi wa nne mfululizo na unaipandisha Azam FC kileleni baada ya kufikisha pointi 12 na kuishusha KMC aliyepoteza mchezo wake uliopita dhidi ya Kagera Sugar juzi na kubaki na pointi tisa.

Awali, mchezo huo ulikuwa wenye kasi kubwa timu zote zikishambuliana kwa zamu kipindi cha kwanza. Kipindi cha pili wote walikuwa kwenye kasi na dakika za lala salama wanalambalamba hao wakafunga bao hilo lililodumu hadi kumalizika kwa mchezo huo.

Aidha, Polisi Tanzania ilitumia uwanja wake wa nyumbani wa Ushirika Moshi kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC.

Mabao ya Polisi Tanzania mawili yalifungwa na Marcel Kaheza katika dakika ya 11 na 61 na lingine lilifungwa na Tariq Seif dakika ya 68. Huo ni ushindi wa kwanza mkubwa kwa Polisi tangu kuanza kwa ligi msimu huu ikifikisha pointi saba sawa na Dodoma Jiji.

KIKOSI cha Yanga chini ya kocha mpya Cedric Kaze kimeendelea ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi