loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Dk. Mabula aahidi kuboresha kituo cha afya

MGOMBEA ubunge wa jimbo la Ilemela kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM),Dk Angelina Mabula ameahidi kuendelea kuboresha kituo cha Afya cha Buzuruga kilichopo katika kata ya Buzuruga,mkoani Mwanza.
Dk Mabula alisema hayo wakati wa mkutano wa kampeni katika viwanja vya shule ya msingi Nyambiti.Dk Mabula alisema wametumia shilingi milioni 400 kwajili ya ujenzi wa kituo hicho ambapo kina sehemu ya Maabara,Mochwari na alisema Jengo la upasuaji litaanza kazi wiki ijayo.Dk Mabula alisema tayari Serikali imetenga shilingi milioni 65 kwajili kukamilisha ukarabati jengo la wagonjwa wa nje.

Dk Mabula alisema wametumia shilingi milioni 10 katika kuweka uzio kwenye kituo  hicho.Dk Mabula aliahiadi kujenga zahanati kwenye katika kata ya Buzuruga.Katika sekta ya Elimu,Dk Mabula alisema wametenga shilingi milioni 46/- kwajili ya ujenzi wa madarasa mawili katika shule ya msingi,Nyambiti na darasa moja katika shule ya msingi Amani pamoja ujenzi wa ofisi ya walimu,Nyambiti.

Dk Mabula alisema wametenga shilingi milioni 80 kwajili ya ujenzi wa barabara za Buzuruga-Makaburini na daraja LA Nundu wametenga shilingi milioni  48 ili liweze kukarabatiwa.

WASIMAMIZI wa vituo na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi,wameonywa kujiepusha na ...

foto
Mwandishi: ALEXANDER SANGA

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi