loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Silaha 600 zakusanywa kutoka kwa raia

KAMATI ya kupunguza silaha katika Jimbo la Warrap, imekusanya silaha 600 kutoka kwa raia tangu Agosti, mwaka huu. Juni, mwaka huu, kamati za usalama ambazo zinajumuisha makamishna wa zamani wa kaunti za Tonj Kaskazini na Tonj Kusini, zilianzisha kampeni ya kuhamasisha wananchi kusalimisha bunduki zao kwa amani kabla ya kuanza kwa msako wa silaha.

Aliyekuwa Kamishna wa Kaunti ya Manaloor, Paul Mangong, ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Usalama Jimbo la Tonj North, alisema wamekusanya silaha 573 katika kanda tatu za kamati hiyo.

“Kwa idadi ya bunduki zilizokusanywa, ambao hawajafanya hivyo hadi sasa, sisi makamishna wa zamani wa amani tutatumia nguvu kuzikamata ili silaha zaidi ziweze kudhibitiwa,” alisema.

Mjumbe wa kamati hiyo, Makuer Tiau, alidai kuna baadhi ya vijana wamekuwa wakiuza bunduki katika kaunti za jirani au kuzificha baada ya msako wa silaha kuanza na kwamba timu hiyo itaendelea na msako huo katika maeneo mengine ya Manyangngok na Ja

foto
Mwandishi: JUBA

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi