loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Marufuku kuuza maeneo ya pwani ya Ziwa Victoria

SERIKALI imepiga marufuku kununua au kuuza maeneo ya pwani mwa Ziwa Victoria, huku shughuli zozote zitakazofanywa katika maeneo hayo bila kuheshimu sheria na mamlaka zikisitishwa.

Uamuzi huo umetangazwa na na Wizara ya Mazingira, Kilimo na Mifugo kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari mwishoni mwa wiki. Katika taarifa hiyo, Waziri wa wizara hiyo, Dk Déo Guide Rurema , alisema hatua hiyo imechukuliwa ili kutoa nafasi kwa timu ya wataalamu watakaoandaa mpango jumuishi wa maendeleo ya pwani ya ziwa hilo.

“Timu ya wataalamu itakuja na mpango maalumu wa kulinda maeneo hayo, ikiwamo utekelezaji wa sheria katika kulinda pwani ya Ziwa Victoria,” alisema.

Alisema mpango huo utazingatia utunzaji mazingira, shughuli za utalii na uchumi, pamoja na kuweka uzio katika maeneo hayo.

“Yeyote aliyezungushia uzio katika maeneo hayo aanatakiwa kuondoa kwa gharama zake katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja, vinginevyo atatozwa faini kulingana na sheria namba 10 na 110 ya maji,” alisema.

foto
Mwandishi: BUJUMBURA

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi