loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Msiuze au kuazimana kadi ya mpigakura

MSIMAMIZI wa Uchaguzi katika Jimbo la Sumbawanga Mjini mkoani Rukwa, Jacob Mtalitinya amewaonya wananchi wanaouza kadi zao za mpigakura kwa siri. Amesema kitendo hicho ni kinyume cha sheria na watakaobainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Mtalitinya ambaye pia ni Mkurugenzi Manispaa ya Sumbawanga alisema hayo alipozungumza na HabariLEO jana katika mahojiano maalumu kuhusu kadi hizo za kupiga kura.

Alisema kuwa zipo taarifa kuwa kuna baadhi ya wananchi wameanza kuuza kadi hizo kisirisiri. Alisema wananchi hao ni wenye sifa ya kupiga kura Oktoba 28 kwamba wamejiandikisha katika daftari la mpigakura.

"Nawaomba wananchi wasiuze viparata (kadi za mpigakura) vyao, ni kinyume cha sheria kwa kuwa ni mali ya aliyejiandikisha kwenye daftari la mpigakura ...vitunzeni kama mnavyotunza vitambulisho vyenu vingine, msirubuniwe hakuna utaratibu wa kuuza, kununua au kuazimana viparata ... Msiwaachie rafiki zenu wala wenza wenu,"alihadharisha.

Alisema amelazimika kutoa hadhari hiyo, kutokana na taarifa baadhi ya watu wanapita nyumba kwa nyumba na mtaa kwa mtaa wakivichukua viparata hivyo, baada ya kuwahadaa wamiliki.

"Lipo linasemwa watu wanauziana kisirisiri, tunakusanya ushahidi ...hatua kali zitachukuliwa kwa watakaobainika,"alisisitiza.

Alisema hadi sasa vyama vyote sita, vinafanya kampeni zao za uchaguzi kwa amani na utulivu, vikinadi ilani zao za uchaguzi kwa wapigakura wao.

Vyama vya siasa vinavyofanya kampeni za uchaguzi katika Jimbo la Sumbawanga Mjini ni CCM, Chadema, CUF, ACT - Wazalendo na NCCR-Mageuzi.

"Vyama vitano tayari vimezindua rasmi kampeni zao za uchaguzi isipokuwa chama cha UDP," alifafanua

WASIMAMIZI wa vituo na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi,wameonywa kujiepusha na ...

foto
Mwandishi: Peti Siyame, Sumbawanga

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi