loader
Dstv Habarileo  Mobile
NBC yaibuka kinara wa maonesho ya madini Geita

NBC yaibuka kinara wa maonesho ya madini Geita

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imeibuka kinara kwenye Maonesho ya Madini na Teknolojia yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mkoani Geita, ambapo taasisi hiyo imefanikiwa kutwaa jumla ya tuzo tatu ikiwemo tuzo ya mshindi wa kwanza kwa taasisi za kifedha na benki zilizoshiriki kwenye maonesho hayo.

Benki hiyo pia ilifanikiwa kutwaa tuzo ya Mdhamini Mkuu wa maonesho hayo kwa taasisi za fedha huku pia ikifanikiwa kuibuka mshindi wa tatu wa jumla katika maonesho hayo.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo hizo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu na Uwekezaji, Angellah Kairuki aliyemwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mkurugenzi wa Idara ya wateja binafsi, Benki ya NBC, Elibariki Masuke alisema tuzo hizo tatu zinaakisi mafanikio makubwa ambayo benki hiyo imeyapata kupitia maonesho hayo.

“Tuzo hizi tatu zinaakisi mafanikio makubwa ambayo Benki ya NBC tumeweza kuyapata kupitia maonesho haya ikiwemo kuendesha programu mbalimbali za mafunzo kwa wadau takribani 600 wa sekta ya madini wakiwemo wachimbaji wadogo na wajasiriamali,’’ alisema.

Aliongeza kuwa mkakati wa benki hiyo baada ya maonesho hayo ni kutekeleza kwa vitendo masuala muhimu iliyoahidi kuyafanya kwa kushirikiana na wadau hao ili kuboresha zaidi sekta hiyo.

Katika maonesho hayo benki hiyo pia iliendesha huduma za kibenki ikiwemo kufungua akaunti mpya kwa wateja, kuendesha kliniki ya biashara ambayo ilisaidia kukusanya maoni ya wadau wa sekta ya madini zaidi ya 150 ambao walikutanishwa na taasisi mbalimbali za serikali.

Aidha kupitia makongamano mbalimbali benki hiyo iliwawezesha wadau wa sekta ya madini kubadilishana mawazo baina yao wenyewe lakini pia baina yao na mamlaka mbalimbali za serikali ikiwemo Wizara ya Madini, TRA, NEMC, SIDO na TANTRADE, TABWA, OSHA,GST na NSSF.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/fe423249c61d494ea33986a0e7ac21c0.jpg

Sehemu kubwa ya ulimwengu wa biashara uli dorora kutokana na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Geita

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi