loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Vyama vyaridhishwa na utendaji kazi wa ZEC

VYAMA vya siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi mkuu, vimesema vimeridhishwa na utendaji wa Tume ya Uchaguzi Mkuu (ZEC) katika kusimamia uchaguzi mkuu na kuvitendea haki vyama vyote vilivyosimamisha wagombea.

Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha NLD, Mfaume Khamis Hassan alisema wameridhishwa kwa kiasi kikubwa na hatua ya uchaguzi mkuu ulivyofikia.

Alisema wanaipongeza ZEC kwa usimamizi mzuri. Alisema zoezi hilo limeratibiwa vizuri kuanzia hatua ya uchukuaji wa fomu katika ofisi za tume hiyo hadi uhakiki wa majina ya wagombea na hatua za mwisho za uteuzi.

‘’Sisi chama cha NLD tumeridhishwa na hatua ya uchaguzi linavyoendeshwa chini ya usimamizi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ZEC kuanzia hatua ya uchukuaji wa fomu hadi urejeshaji na baadaye kuhakiki wagombeya kuelekea uchaguzi mkuu,’’ alisema.

Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Ada Tadea, Juma Ali Khatib aliipongeza Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kwa kuvishughulikia vyama vyote vya siasa vilivyoweka wagombea wa urais bila ya kujali kuwepo kwa vyama vikubwa.

Alisema hatua hiyo imetoa faraja kubwa kwa vyama vya siasa, kupata matumaini kwamba uchaguzi mkuu wa Oktoba 28 utakuwa huru na haki na kutoa nafasi kwa aliyeshinda kukabidhiwa madaraka.

‘’Sisi vyama vya siasa tumefarijika kwa kiasi kikubwa jinsi uchaguzi mkuu unavyoratibiwa na Tume ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) bila ya kuegemea vyama vya siasa ikiwemo vile vinavyoitwa vikubwa,’’alisema

WASIMAMIZI wa vituo na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi,wameonywa kujiepusha na ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi