loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mgombea urais DP kujenga viwanda Micheweni

MGOMBEA Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha DP, Shafi Hassan Suleiman amesema akishinda atajenga viwanda vikubwa vya kusindika samaki na mazao ya baharini katika maeneo huru ya uchumi yaliyopo Micheweni kisiwani Pemba.

Alisema hayo alipozungumza na wananchi na wafuasi wa chama hicho katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho huko Micheweni.

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imeyatenga maeneo huru ya uchumi katika eneo la Micheweni tangu mwaka 1992 bila ya kuyatumia.

‘’Nikichaguliwa kuwa rais wa Zanzibar nakusudia kuyatumia maeneo huru ya uchumi yaliyopo Micheweni Pemba kwa kujenga viwanda vikubwa vitakavyozalisha ajira,’’ alisema.

Aidha, alisema chama chake kinawataka wanachama na wafuasi wake, kudumisha amani na utulivu katika kipindi chote ili taifa liwe na utulivu.

Alisema Wazanzibari wamechoka na vurugu za kisiasa zinazojitokeza kabla ya uchaguzi na mara baada ya uchaguzi mkuu na kuwaweka wananchi katika hofu na wasiwasi mkubwa.

‘’Chama cha DP kinawataka wanachama na wafuasi wake kuwa watulivu katika kipindi hichi kuelekea uchaguzi... msikubali kurubuniwa kushiriki katika vurugu za kisiasa zinazotokana na jazba,’’ alisema.

Mapema, Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano katika chama hicho, Zaina Juma Khamis aliwataka wananchi wajenge matumaini makubwa kwa chama chao, ambacho kimejipanga kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati.

‘’Wananchi mkituchagua tutaharakisha maendeleo kwa wananchi na kuongeza ajira katika miradi mikubwa,’’ alisema.

WASIMAMIZI wa vituo na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi,wameonywa kujiepusha na ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi