loader
Dstv Habarileo  Mobile
Taasisi ya Uhasibu kufunza teknolojia mawakala fedha

Taasisi ya Uhasibu kufunza teknolojia mawakala fedha

MAWAKALA wa fedha wa benki mbalimbali mitaani na wa mitandao ya simu ni miongoni mwa walengwa wa mafunzo maalumu katika Taasisi ya Uhasibu Arusha (IAA) Kampasi ya Dar es Salaam ili kuendesha biashara zao kisasa zaidi na kukuza mitaji.

Mkuu wa IAA, Profesa Eliamani Sedoyeka, alisema mwishoni mwa wiki kuwa taasisi hiyo pia ipo mbioni kutoa mafunzo kwa wanahabari itakayowezesha mwandishi mmoja wa habari kuzalisha habari na kuisambaza kupitia magazeti, redio, televisheni na mitandao ya kijamii bila kulazimika kuambatana na mwingine na kuwahi muda.

Akizungumzia mafunzo hayo kuhusu benki, Profesa Sedoyeka alisema yamelenga kuandaa vijana kuwa watoa huduma za benki kwa vitendo ili kuleta mapinduzi katika sekta ya benki kwa kuwa nusu ya muda mafunzo yatafanyika darasani na nusu nyingine yatakuwa kwa vitendo katika benki.

“Kozi hii ya digrii ya kwanza inalenga sekta ya kibenki ikihusisha pia wafanyabiashara wadogo ili wakaanzishe biashara na kuiboresha kwa kukuza mitaji na ikibidi sasa watoke kuwa wakala wa benki na mitandao ya M-Pesa, Tigo- Pesa, Halo-Pesa, T-Pesa na nyingine, sasa waanze hata kutoa mikopo midogomidogo maana fedha zinataka utaalamu maalumu,” alisema.

Akizungumzia wanahabari, alisema programu inayowahusu ya ‘multimedia’ ipo katika ngazi ya astashahada na shahada.

“Hii ni kozi mpya katika Taasisi ya Uhasibu Arusha Kampasi ya Dar es Salaam inayokusudia kumfanya mwanahabari wa kisasa kuwa ‘jeshi la mtu mmoja’ yaani, akienda kwenye tukio awe na uwezo wa kuchukua habari na picha, kuhariri, kuandika maelezo ya picha fupi inayovutia na kueleweka; aipandishe habari kwenye blogu yake au ‘oline TV’ na ikibidi, huyo huyo aipeleke kwenye redio au gazeti lao.”

Aliongeza: “Taasisi imechunguza na kubaini ukweli kuwa, uandishi wa habari wa sasa ni tofauti na ule wa zamani na watumiaji wa habari wanabadilika kwa kuendana na wakati na kukua kwa teknolojia; wanataka habari za haraka, fupi, zinazoeleweka na zenye vionjo hivyo, ndiyo maana tumeona ni lazima kuandaa mwandishi wa habari wa kisasa ili pia vijana wajiandae kujiajiri au kuajiriwa na hapa watafundishwa maadili ya taaluma, mbinu na ujuzi katika uandishi wa habari.”

Hivi karibuni iliripotiwa kuwa IAA imeanzisha Programu ya Menejimenti ya Biashara na Kichina kwa ngazi za astashahada na stahashada katika Kampasi ya Dar es Salaam ili kuwapa watanzania fursa za ajira na biashara katika miradi mbalimbali inayohusisha Wachina.

Aidha, imeanzisha kozi fupi inayolenga kuwasaidia wajasiriamali wa kawaida na yeyote mwenye wazo la kuwa mjasiriamali kujua mambo muhimu ya biashara yakiwamo ya utunzaji wa kumbukumbu, namna ya kuandaa andiko la mradi, kukuza mtaji, kupata soko, kuwekeza na kuweka akiba.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/5cd7457f2be0ddf00b32fdb0aa52e506.jpg

Sehemu kubwa ya ulimwengu wa biashara uli dorora kutokana na ...

foto
Mwandishi: Joseph Sabinus

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi