loader
Dstv Habarileo  Mobile
Watoboa siri ya kuanza kulima korosho

Watoboa siri ya kuanza kulima korosho

WAKULIMA wa tumbaku mkoani Mbeya, wameanza kulima korosho kama zao mbadala la kibiashara, kutokana na tumbaku kukosa soko la uhakika na uharibifu wa mazingira katika kilimo hicho.

Walibainisha hayo walipozungumza na waandishi wa habari, kwenye mafunzo yao ya kilimo bora cha zao la korosho pamoja na maofisa ugani wa wilaya za Chunya na Kyela.

Mafunzo hayo yaliandaliwa na Kituo cha Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Naliendele na Bodi ya Korosho. Walisema zao la tumbaku ambalo walikuwa wanalitumia kama zao la kibiashara limeshuka sana.

Hivyo, walisema hatua ya kupewa elimu na mbegu bora za korosho, itabadilisha kilimo chao ili kiendelee kuwasaidia kiuchumi.

Mkulima kutoka Wilaya ya Chunya, Sailis Mendrad alisema wamehama kutoka zao la tumbaku na kuanza kulima korosho, kutokana na tumbaku kuwa na changamoto nyingi ikiwemo kukosa soko hivi sasa.

Alisema wameamua kulima korosho, kutokana na kuwa zao hilo linafanya vizuri sokoni hivi sasa hivyo wameona ni vema kulifanya kuwa la biashara.

Mkuu wa Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Cuthbert Mwinuka alisema kilimo cha korosho kilianzishwa wilayani hapo kama zao mbadala, baada ya kuona kuwa soko la tumbaku linaendelea kushuka mwaka hadi mwaka.

Mwinuka alisema walianza kuzalisha korosho kwa vijiji 27 mwaka 2017/18 . Walipata mbegu kilo 344 na kuzalisha miche 32,000. Walipata wakulima 627 walioanza kuzalisha ili wengine waige kutoka kwao.

Mwaka 2019 walipata tani tano za mbegu na zilizalisha miche 10,000 na kupandwa na wakulima 5,656. Mwaka 2019/20 walipata mbegu kilo 3,340 na kupata miche 200,052 na wakulima 2,130 walipanda.

Hadi sasa wakulima 8,386 wamepanda ekari 15,845 na miche iliyopandwa mpaka sasa ni 752,248. Kiasi cha mbegu ambacho kiliingizwa ni kilo 8,974.

Mratibu wa Uhaulishaji wa Teknolojia na Uhusiano kutoka TARI Naliendele, Bakari Kidunda alisema wanajivunia kituo chao kuwa moja ya vituo bora vya utafiti wa zao la korosho barani Afrika na dunia kwa ujumla.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/fa822c8786ebccd7bd7d58a9838db751.jpg

Sehemu kubwa ya ulimwengu wa biashara uli dorora kutokana na ...

foto
Mwandishi: Agnes Haule, Mbeya

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi