loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Pato la ndani EAC lapiku jumuiya nyingine kikanda

BAJETI ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa mwaka wa fedha 2020/2021 ya dola za Marekani milioni 97.7 hatimaye imewasilishwa katika Bunge la jumuiya hiyo (EALA), huku ikionesha kumekuwa na ukuaji mkubwa wa Pato la Ndani hadi  kufikia asilimia 5.9.

Bajeti hiyo iliyowasilishwa katika bunge hilo Ijumaa iliyopita Septemba 25, imejikitazaidi katika kukabiliana na madhara yaliyojitokeza kutokana na mlipuko wa virusi vya corona katika ukanda huo.

Kwa mujibu wa bajeti hiyo mwaka wa fedha uliopita,Pato la Ndani la EAC limekuwa kwa kiasi kikubwa hadi kufikia asilimia 5.9, ikiwa ni kubwa zaidi kati ya jumuiya zote za kiuchumi za kikanda barani Afrika.

Akiwasilisha makadirio ya bajeti hiyo,Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki,Manasseh Nshuti, alisema katika ya fedha hizo, dola za Marekani milioni 55 sawa na asilimia 57,zitachangiwa kwa usawa na nchi wanachama au mapato ya ndani na dola za Marekani milioni 41 sawa na asilimia 43 zitapatikana kutoka kwa wadau wa maendeleo.

Alisema bajeti hiyo yenye kauli mbiu ya ‘Kuchochea uchumi kulinda maisha, ajira, biashara na viwanda, itasaidia kuleta ahueni ya kiuchumi katika  ukanda huo  kutokana na changamoto za ugonjwa wa covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona.

Hata hivyo, Nshuti alisema bajeti ya mwaka huuimeshuka ikilinganishwa naya mwaka wa fedha 2019/2020 ambayo Bunge la EALAlilipitisha dola za Marekani 116,428,004.

Alitaja vipaumbe vya bajeti hiyo kuwa nikukuza maendeleo ya viwanda kikanda kupitia uwekezaji katika sekta muhimu za vipaumbele, ukuzaji ujuzi, maendeleo ya teknolojia na uvumbuzi, ili kuchochea maendeleo ya uchumi.

Alisema katika kilimo, EAC imeweka mikakati ya kuboresha  kilimo chenye tija, kuongeza thamani ya mazao na kuwezesha usafirishaji wa bidhaa za kilimo ili kuongeza usalama wa chakula katika ukanda huo.

“Madhara ya ugonjwa huu kwa nchi wanachama wa EACingawa bado haijafanywa tathimini lakini hakuna ubishi kuwa ni makubwa,”alisema.

Alisema bajeti hiyo itajikita katika kutekeleza programu mbalimbali za kipaumbele, ikiwamo kuwa na eneo moja la forodha (SCT) kwa ajili ya kuingiza bidhaa kutoka nje na zinazouzwa ndani ya EACna bidhaa nyingine zinazotumiwa kwa wingi EAC na  maendeleo ya miundombinu.

Akitoa mchanganuo wa bajeti hiyo, Nshuti alisema pia imetengwa kuhudumia vyombo vikuu na taasisi za EAC, ambapo  Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki imetengewa zaidi ya dola za Marekani milioni 48.564, Bunge la EALA zaidi ya dola za Marekanimilioni 16.755 na Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki zaidi ya dola za Marekani milioni 3.970.

Nyingine ni Baraza la Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki lililotengewa zaidi ya dola za Marekani milioni 10.977,  Tume ya Bonde la Ziwa Victoria zaidi ya dola milioni 8.380,  wakati zaidi ya dola milioni 3.077 zimetengwa kwa Shirika la Uvuvi la Ziwa Victoria.

Tume ya Sayansi na Teknolojia ya Afrika Mashariki imetengewa zaidi ya dola za Marekani milioni 1.536, Tume ya Kiswahili ya Afrika Mashariki zaidi ya dola milioni 1,399, Tume ya Utafiti wa Afya ya Afrika Mashariki zaidi ya dola za Marekani milioni 1.879, wakati Mamlaka ya Ushindani  ya Afrika Mashariki imetengewa zaidi ya dola milioni 1.128.

Kuhusu bajeti ya mwaka wa fedha uliopita,Nshutialisema  Pato la Ndani la EAC  limekua mwaka jana kwa asilimia 5.9 kutoka asilimia  5.7 za mwaka 2018 na asilimia 5.6 mwaka  2017.

“Ukuaji huu ni mkubwa zaidi  kati ya jumuiya zote za kiuchumi za kikanda barani Afrika,” alisema.

Katika miundombinu, Nshuti alisema EAC inaendelea NA ujenzi wa vituo vya kutoa huduma kwa pamoja mipakani vya Nimule/Elegu (mpaka wa Uganda na Sudan Kusini ) na Tunduma (Tanzania na Zambia Zambia ),iliyozinduliwa mwaka wa fedha uliopita.

Alisema ujenzi wabarabara ya kilometa 400 ya Tanzania-Kenya inayopita Malindi -Lunga Lunga na Tanga kupitia Bagamoyo,upo katika hatua ya zabuni baada ya kupata ufadhili wa euro milioni 375 kutoka Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) na Umoja wa Ulaya (EU).

Kuhusu barabara ya Kabingo- Kasulu -Manyovu ya kilometa 260 nchini Tanzania na Gitaza - Rumonge kilometa 45 nchini Burundi, ambayo itaunganisha nchi hizo mbili ujenzi wake utaanza hivi karibuni baada ya kupata misaada na mikopo kutoka AfDB.

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi