loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Samia: Tuchagueni tuna jambo letu

MGOMBEA Mwenza wa urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amewaomba Watanzania wairudishe madarakani Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuwa bado ina kazi ya kuijenga Tanzania.

Amesema serikali tangu iingie madarakani,imetekeleza miradi mingi ya maendeleo katika kila eneo nchini.

Alitaja baadhi ya maendeleo yaliyotekelezwa na serikali hiyo kuwa ni ujenzi wa miundombinu, uboreshaji wa elimu kupitia mpango wa elimu bure, kuboresha afya kwa kujenga hospitali, vituo vya afya na zahanati lakini pia kuhimiza matumizi ya bima ya afya.

Samia aliyasema hayo katika mkutano wa kampeni, uliofanyika eneo la Galapo Babati Mjini.

Alitoa mfano mkoani Manyara kuwa imetekeleza miradi ukiwemo ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami na changarawe. Aliahidi kuwa endapo CCM itapewa ridhaa ya miaka mitano ijayo, itaiboresha zaidi Mfuko ya Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (Tarura).

Alisema pia mkoani humo, serikali iliweka taa za barabarani za sola 219 zilizofungwa katika Halmashauri ya Mji Babati na Mbulu kwa Sh milioni 49.

“Tutaendelea na ujenzi wa miundombonu mbalimbali Manyara kurahisisha usafiri na usafirishaji wa mazao.Tunajua hapa Manyara kuna wakulima na wafugaji miundombinu ni muhimu sana,”alisema Samia.

Alitaja maendeleo mengine yaliyotekelezwa mkoani humo kuwa ni maji na kusisitiza kuwa bado tatizo la maji ni changamoto katika maeneo mengi nchini na kwamba, serikali ya CCM imepanga kuimaliza kabisa.

“Upatikanaji wa maji vijijini umeongezeka asilimia 52 mwaka 2015 hadi asilimia 58 mwaka huu. Bado hali si nzuri sana hata nikiwa njiani nimeona. Miji midogo umeongezeka kutoka asilimia 58 hadi 78, mijini asiliamia 74 hadi 87,” alieleza.

Alisema serikali inatambua changamoto ya maji na miaka inayokuja imepanga kuhakikisha inamaliza tatizo hilo ikiwemo kujenga mabwawa katika maeneo ambayo kima cha maji kiko chini sana. “Ilani inasema vijijini maji yatapelekwa kwa asilimia 85 na mijini asilimia 95,”.

Kuhusu huduma za nishati alisema kwa Manyara pekee jumla ya vijiji 218 vimeunganishwa kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) na jumla ya Sh bilioni 37.6 zilitumika.

Alisema serikali hiyo imeunganisha vijiji hivyo kutoka vijiji 13 mwaka 2015 hadi 231 mwaka huu.

Bado vijiji 165 vitakavyopatiwa umeme wa REA ya tatu mzunguko wa tatu mkoani Manyara na zabuni zimeshatangazwa ambapo vijiji 30 vitamaliziwa katika mwaka wa fedha 2021/22.

Alisema CCM ikipata ridhaa itaendeleza mpango wake wa elimu bure ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya shule na kujenga madarasa mapya.

Kuhuau afya alisema, sera ya kujenga vituo vya afya katika kila kata na zahanati katika kijiji itaendelezwa na kukamilishwa.Hata hivyo, alionesha kusikitishwa na idadi ndogo ya Watanzania kujiunga na bima ya afya.

“Naambiwa hapa Manyara ni asilimia mbili tu ya watu ndio waliojiunga na mfumo wa bima ya afya, hii si nzuri. Bima ya afya inakuwezesha kupata huduma za afya wakati wowote bila kuwa na hofu ya kuwa na fedha,” alisema.

Watanzania 4,247 wamepata ...

foto
Mwandishi: Halima Mlacha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi