loader
Dstv Habarileo  Mobile
Majaliwa ataka wananchi  wasidanganywe bei ya kahawa

Majaliwa ataka wananchi wasidanganywe bei ya kahawa

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amesema Serikali ya CCM imedhamiria kuhakikisha kilimo kinamnufaisha mkulima. 

Ametoa kauli hiyo jana alipohutubia wakazi wa Rubale kwenye mkutano katika viwanja vya Shule ya Msingi Rubale wilayani Bukoba, mkoani Kagera.

"Watu wasije kuwadanganya kwamba serikali haiwajali, siyo kweli. Kuna sababu zilizochangia kuyumba kwa bei ya kahawa kwenye soko la dunia."alisema Majaliwa na kuongeza;

"Serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani, iliazimia kufufua mazao matano ya kimkakati ambayo ni kahawa, pamba, korosho, chai na tumbaku. Mazao haya bei ilishuka na si katika zao la kahawa tu."

Alisema, kuyumba kwa bei haikuwa katika zao la kahawa tu, bali mazao mengine ikiwemo pamba na korosho. 

“Kahawa bei yake iliathirika kwa sababu ya ugonjwa wa corona. Korosho bei ilishuka kutoka shilingi 3,300 hadi shilingi  1,900. Pamba pia ilishuka bei," alisema Majaliwa. 

Alisema, mnada wa kahawa hufanyika Kenya lakini hadi sasa bado wanasumbuliwa na ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona kwa hiyo haikuwa rahisi kufanya biashara.

Katika mkutano huo, Majaliwa alimuombea kura Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, John Magufuli, mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM, Jason Rweikiza, mgombea udiwani wa kata ya Rubale, Rwegasira Rwechungura na madiwani wengine kwenye jimbo hilo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/af1e4bdebdc9c46cee3ec26318483936.JPG

Sehemu kubwa ya ulimwengu wa biashara uli dorora kutokana na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalum

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi