loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waandishi TSN wang’ara

WANDISHI watatu wa Kampuni ya Magazeti ya Tanzania Standard Newspapers (TSN), inayozalisha magazeti ya Daily News, HabariLeo na SpotiLeo wameng’ara Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) mwaka 2019.

Wandishi hao ni  Sauli Gilliad wa  Daily News ambaye ameshinda Tuzo ya Wazi,  Baraka Messa ameshinda Tuzo ya Masuala ya Kilimo na Biashara wakati Lasteck Alfred ameshinda Tuzo ya Masuala ya Uchunguzi.

Waandishi wengine ambao waliteuliwaa kushiriki tuzo hizo  ni Evance Ng’ingo wa HabariLeo Dar es Salaam, Lucas Raphael kutoka Tabora, Sifa Lubasi kutoka Dodoma, Kareny Masasy wa HabariLeo Shinyanga, James Kamala kutoka gazeti la Daily News Dar es Salaam ambao wameshika nafasi ya pili.

Sherehe za tuzo hizo zilifanyika hoteli ya Tanga Beach Resort jana.

Mshindi wa jumla aliyeibuka ni  Halili Letea wa Mwananchi na Hilda Phoya wa Mlimani TV ambao wameshinda  Tuzo ya Jumla ya Umahiri wa Uandishi wa Habari (EJAT) 2019.

Washindi hao wawili wamepata tuzo, cheti na mfano wa hundi wenye thamani ya Shilingi milioni tatu  kila mmoja na walikabidhiwa kitita hicho na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela.

Kwa mujibu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) hii ni mara ya pili kwa washindi wa jumla wa tuzo hizo za EJAT, kuwa watu wawili.

Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2014, ambapo Lucas Liganga na Mkinga Mkinga, wote kutoka gazeti la The Citizen, waliibuka washindi wa jumla baada ya kushinda tuzo ya uchunguzi kwa kuibua skendo ya Tegeta Escrow.

Washindi wengine katika tuzo hizo za EJAT 2019 ni Neema Goyayi wa AFM Radio Dodoma na Fatma Chikawe wa Azam TV upande wa kipengele cha  michezo na utamaduni.

Tuzo ya Wazi imekwenda kwa Amina Semagogwa wa Radio Kwizera  na  Sauli Gilliad wa  Daily News.

Aliyeshinda Kipengele kipya cha  Athari za Kemikali kwa Afya na Mazingira upande wa gazeti ni Gwamaka Alipipi wa Nipashe, na Damian Macha wa Fountain Radio kwa upande wa redio. Kwa upande wa televisheni aliyeibuka kidedea ni Agnes Almasi wa ITV, aliyefariki hivi karibuni. 

Tuzo ya Biashara na Uchumi ameshinda Hilda  Phoya wa Mlimani TV wakati kwa upande wa  Radio, ameshinda Asha Ahmed Omar wa Chuchu FM Zanzibar.

Tuzo ya Mafuta, Gesi na Usimamizi wa Sekta ya Madini, imenyakuliwa na Halili Letea wa The Citizen wakati Sanula Athanas wa Nipashe ameshinda Tuzo ya Utalii na Uhifadhi wakati kwa upande wa redio ameshinda Rajabu Mrope.

Sanula pia ameshinda tuzo ya Utawala Bora upande wa gazeti, Joseline Kitakwa wa  TBC FM ameshinda tuzo ya Biashara na Uchumi na Jamaly Hashim wa Azam Tv ameshinda tuzo hiyo upande wa TV na Baraka Messa wa Habari leo ameshinda upande wa gazeti.

Khamis Suleiman wa  Channel Ten ameshinda Tuzo ya Mpigapicha  huku Abdul Kingo wa The Guardian ameibuka kidedea tuzo ya Katuni upande wa gazeti.

Adella  Tillya wa  EFM  na Agnes Mbapu wa  TBC wameshinda Tuzo wa Afya  ya Uzazi kwa upande wa TV na redio wakati kwa upande wa gazeti ameshinda Christina Mwakangale wa Nipashe.

Tuzo ya masuala ya elimu upande wa redio ameshinda  Anord  Kailembo wa Radio Kwizera, na Faraja  Sendegeya wa Azam TV  na  Halili  Letea wa  Mwananchi ameshinda upande wa gazeti.

Waandishi wawili wa Radio Sauti ya  Yohanne Gwangway  na  Dominic Mrimi wameshinda tuzo ya takwimu kwa upande wa gazeti ameshinda Halili Letea wa  Mwananchi.

Herieth Makweta na Godfrey Kahango  wote wa Mwananchi wameshinda tuzo ya habari za watoto wakati Hilda Phoya wa Mlimani ameshinda tuzo hiyo kwa upande wa TV.

Vipengele vingine vilivyoshindanishwa ni hedhi salama na usimamizi wa usafi ameshinda Rehema Matowo wa Mwananchi upande wa gazeti, Faraja Sendegeya wa Azam TV na Adam Gabriel wa Radio  CG FM.

Tuzo ya Masuala ya Jinsia imechukuliwa na Rahma  Ali wa ZanzibarLeo na Hadija Omari Nasoro wa  Voice of Tabora.

Tuzo ya Usalama Barabarani upande wa gazeti ameshinda Crispin Samson wa The Guardian, Hilda  Phoya wa Mlimani TV na  Anord  Kailembo.

Kipengele kipya cha ubunifu na maendeleo ya binadamu, imechukuliwa na Philip Mwihava wa Clouds FM na Tatu Kazimoto wa TBC

WASIMAMIZI wa vituo na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi,wameonywa kujiepusha na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi