loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

NEC kufikiria waliopoteza vitambulisho vya kupiga kura

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeahidi kulifanyia kazi ombi ya wadau wa uchaguzi kwamba wananchi waliopoteza vitambulisho vya kupigia kura watumie vitambulisho vingine vinavyotambulika kitaifa kupiga kura.

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa (NEC), Giveness Aswile alitoa ahadi hiyo wakati akijibu ombi la Chifu Lazaro Mahoma aliyeomba NEC iwape wananchi fursa ya kupiga kura hata waliopoteza vitambulisho vya mpiga kura.

Chifu Chihoma alihoji NEC itamsaidiaje mpiga kura ambaye amepoteza kitambulisho anayetaka kutumia haki yake ya kumpigia kura Rais, mbunge na diwani kwa kupiga kura kutumia vitambulisho vingine.

Aswile ambaye ni Mkurugenzi wa NEC anayeshughulikia Habari na Elimu kwa Mpigakura alisema, NEC imesikia ombi hilo italifanyia kazi ili kuona kama kuna uwezekano kwa waliopoteza vitambulisho vya mpiga kura kutumia vitambulisho vingine.

Vitambulisho vingine vinavyoweza kutumika kama mpigakura atakuwa amepoteza kitambulisho cha mpiga kura ni kitambulisho cha taifa, leseni ya udereva au pasi ya kusafiria.

Mdau mwingine, John Mchenya alihoji NEC itasaidiaje watu watakaopata changamoto ya kuchelewa kufika vituo siku ya uchaguzi, je wataruhusiwa kupiga kura mahali pengine.

Mwanasheria wa Tume, Fausta Mahenge alisema kwa mujibu wa sheria na kanuni za uchaguzi zinamtaka mpigakura kupiga kura kupata katika kituo alichojiandikisha kwa kuwa ndipo lilipo jina lake.

Tangu Septemba 28, hadi Oktoba 7 mwaka huu NEC itakuwa ikifanya mikutano na wadau wakiwemo viongozi wa kidini, taasisi za kidini, asasi za kiraia na viongozi wengine ili kuandaa mazingira bora ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 28, mwaka huu.

WASIMAMIZI wa vituo na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi,wameonywa kujiepusha na ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi