loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

‘Waliojimilikisha maeneo ya umma waondoke haraka’

MKUU wa Wilaya ya Dodoma, Josephat Maganga amewataka watu waliojimilikisha maeneo ya umma wilayani humo kuyaacha na kuondoka haraka.

Alitoa agizo hilo hivi karibuni wakati akiwa ziarani katika Kata ya Chahwa kujitambulisha na kusikiliza kero za wananchi. Alisema suala la ardhi liko chini ya sheria kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania ili kuwezesha watu kuishi kwa amani na kwamba, hakuna mtu aliye juu ya sheria.

Aliwataka waliojimilikisha maeneo yaliyotambuliwa kwa matumizi ya umma yakiwamo ya masoko, mabwawa, viwanja vya michezo, gulio la ng’ombe na lambo la serikali waondoke mara moja.

Akahoji: “Maeneo ambayo watu walijimilikisha waondoke mara moja; hivi hawa wanataka tukitaka kuwekeza twende kununua upya maeneo kwa watu?” Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya huyo, kila mtu anapaswa kufuata taratibu na sheria kuhusu matumizi ya ardhi ili kuepusha migogoro ya ardhi inayoweza kuepukwa kwa kutumia busara.

Alisema lengo lake lingine la ziara hiyo lilikuwa kuangalia miradi ya wananchi inayoendelea katika maeneo hayo na kubaini kero zilizopo ili zitafutiwe ufumbuzi.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi katika kata hiyo, Ogra Mtundu alisema changamoto kubwa inayowakabili ni ukosefu wa shule ya hali inayowafanya wanafunzi kutembea umbali mrefu kwenda katika shule za sekondari wanazopangiwa, hivyo ni vyema suala la kuwa na shule ya kata lipewe kipaumbele.

WASIMAMIZI wa vituo na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi,wameonywa kujiepusha na ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi