loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Samia ataka viongozi nchini kudumisha amani

MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi ngazi za chini kudumisha amani na ushirikiano kati yao kama njia pekee ya kuwafi kishia wananchi maendeleo.

Aidha, amesema ingawa nchi ina mfumo wa vyama vingi, hadi sasa chama pekee chenye huruma kwa wanyonge wa nchini ni CCM ndio maana wanaomba ridhaa ya kuongoza tena kwa miaka mitano ili kuendelea kupeleka maendeleo kwa wananchi.

Samia aliyasema hayo jana katika mkutano wa kampeni Bashnet mkoani Manyara na aliomba wapiga kura wasifanye makosa Oktoba 28, mwaka huu kuchagua mchanganyiko, bali wachague kwa mfumo wa mafiga matatu; Rais, wabunge na madiwani wa CCM.

“Utawala bora uzingatiwe, kila mmoja ajue misingi ya kazi yake kuanzia kijiji, tarafa na kuendelea, tusivutane wala kunyang’anyana madaraka, tutazuia maendeleo, kukiwa na hila na kwingine kumenyooka lazima migongano iwepo” alisema Samia.

WASIMAMIZI wa vituo na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi,wameonywa kujiepusha na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi