loader
Mourinho awaangukia  makocha wa taifa

Mourinho awaangukia makocha wa taifa

KOCHA wa Tottenham Hotspur, Jose Mourinho, amewataka makocha wa timu za taifa kuwalinda wachezaji wa timu yake wakati wa mechi za kimataifa zinazokuja wiki za hivi karibuni.

Spurs wanatakiwa kucheza hadi mechi tatu kwa wiki wakati wakisaka nafasi ya kufuzu kwa mashindano ya Ligi ya Ulaya, huku pia wakikabiliwa na mechi za Ligi Kuu na Kombe la Ligi.

“Natumaini makocha wa timu za taifa wana takwimu zao na watabaini wachezaji wa Tottenham wamecheza mechi ngapi wiki hii,” alisema Mourinho baada ya Spurs kuifunga Chelsea kwa penalti katika Kombe la Ligi Jumanne.

“Natumaini wanawajali wachezaji na watawalinda kwa sababu Tottenham wiki hii watakuwa na dakika nyingi za kucheza na kucheza katika mazingira hatari.”

Mourinho alisema aliamua `kujilipua’ kwa kumuanzisha Eric Dier siku mbili baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa England kucheza dakika zote 90 katika mchezo wa Ligi Kuu ambao walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Newcastle United.

Spurs itakabiliana na Maccabi Haifa katika raundi ya mwisho ya kufuzu kwa Ligi ya Ulaya leo Alhamisi kabla ya kuifuata Manchester United katika ligi Jumapili.

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi