loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Urusi yatetea operesheni yake Syria

WAZIRI wa Ulinzi nchini Urusi, Sergei Shoigu amesema operesheni ya Urusi dhidi ya ugaidi Syria ilikuwa ni ya lazima, kwani ilisaidia kuilinda nchi hiyo lakini pia kudhibiti kundi la kigaidi la Islamic.

“Wakati mwingine unasikia swali linaibuka likihoji kama Urusi ilifanya vyema kujibebea mzigo huu wa Syria. Lakini kila swali linapoibuka jibu ni moja, operesheni ya Syria ilikuwa ni ya lazima na muhimu na uamuzi wa kuianzisha operesheni hiyo ulikuwa sahihi na labda ndio ulikuwa uamuzi pekee,” alisema Shoigu.

Shoigu aliyasema hayo katika moja ya mahojiano aliyofanyiwa na gazeti la Wizara ya Ulinzi, lilioandaliwa maalumu kwa ajili ya maadhimisho ya miaka mitano ya operesheni za Urusi nchini Syria.

Operesheni ya Urusi nchini humo ya hivi karibuni ilifanyika kwa siku 804 kuanzia Septemba 30, mwaka 2015 hadi Desemba 11, mwaka 2017.

Kabla ya operesheni hiyo kuanzishwa magaidi walidhibiti takribani asilimia 70 ya Syria na walikuwa wakikabili maeneo mengine mbalimbali huku vikosi vinavyounga mkono serikali vikilazimika kujiondoa.

“Kuna wakati ilikuwa dhahiri kwamba hili kundi la kigaidi ni tishio si tu kwa nchi hiyo bali dunia nzima ikiwemo Urusi. Ni kundi lililopanga kulazimisha binadamu wote walitii,” alieleza waziri huyo.

Kwa msaada wa usafiri wa anga wa Urusi, vikosi vya Syria vilifanikiwa kuyaweka huru maeneo 1,024 kutoka mikononi mwa magaidi. Na matokeo yake vikosi vya serikali navile vya ulinzi vilifanikiwa kurejesha na kudhibiti asilimia 88 ya nchi hiyo.

Alisema Urusi ilifanikiwa kudhibiti kubomolewa kwa nchi ya Syria, kuzuia vita vya wenywe kwa wenyewe lakini kudhibiti kikosi cha kigaidi cha Islamic na kuziba mianya na mtandao wa magaidi.

Alitaja mafanikio ya operesheni hiyo kuwa ni kudhibiti watu zaidi ya 3,000 waliokuwa na hati za kusafiria za Urusi waliojiunga na wapiganaji wa kigaidi Syria kuingia Urusi kutekeleza shughuli zao kigaidi.

“Kazi ilitolewa na Amiri Jeshi Mkuu miaka mitano iliyopita imefanikiwa. Kundi la kigaidi la Islamic lililokuwepo Syria limesambaratishwa na hakuna gaidi aliyeweza kujipenyeza Urusi,” alisema waziri Shoigu.

Waziri huyo alisema kuwa mafanikio mengine muhimu ya operesheni ya Urusi ni kizuizi cha kuaminika ambacho kinazuia vikundi vya kigaidi kuenea katika maeneo mengine, haswa nchi za jirani.

Zaidi ya magaidi 133,000 wameuawa nchini Syria tangu Urusi izindue operesheni yake nchini humo.

WANACHAMA wa Chama cha Republican nchini ...

foto
Mwandishi: MOSCOW, Urusi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi