loader
Dstv Habarileo  Mobile
UBA yaahidi kuendelea kusaidia miradi, mipango

UBA yaahidi kuendelea kusaidia miradi, mipango

MKURUGENZI Mtendaji wa United Bank For Africa (UBA) Tanzania, Kingsley Ulinfun inayofanya biashara kwenye nchi 20 barani Afrika amesema benki hiyo itaendelea kusaidia miradi na mipango ya serikali kupitia ufadhili.

Ulinfun alisema hayo alipomtembelea Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango Mjini Dodoma jana. Wakati wa ziara hiyo, UBA ilipata fursa ya kujadili maendeleo na mipango endelevu ya benki hiyo kusaidia ukuaji wa uchumi wa serikali na ustawi wa jumla wa raia wa Tanzania.

Mkurugenzi wa UBA na Waziri Mpango wamezungumzia miradi ambayo benki hiyo inafadhili na kutoa mikopo ukiwemo wa hivi karibuni wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wa kuzalisha umeme wa megawati 2,115 wa Julius Nyerere wa Mto Rufiji (JNHPP) kwa kutoa Dhamana ya Benki ya Dola za Marekani milioni 366.

Katika nchi nyingine barani Afrika, UBA imeunga mkono mipango kadhaa ya serikali ikiwa ni pamoja na miradi ya umeme, michezo na maboresho ya miundombinu katika nchi za uwepo.

United Bank For Africa ni moja ya waajiri wakubwa katika sekta ya kifedha katika bara la Afrika, ikiwa na zaidi ya wafanyakazi 20,000.

Benki hii inahudumia zaidi ya wateja milioni 20, huku ikiwa na zaidi ya matawi 1,000 na zaidi ya ATM 30,000, PoS na mawakala barani Afrika.

Ikiwa inafanya biashara kwenye nchi 20 za Kiafrika na ulimwenguni kote ikiwemo, Uingereza, Marekani na Ufaransa, UBA hutoa huduma za benki za

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/70e0ab857003a91fdf1ae7c936033cca.jpg

Sehemu kubwa ya ulimwengu wa biashara uli dorora kutokana na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi