loader
Dstv Habarileo  Mobile
Missenyi umeme bado vijiji vinne tu

Missenyi umeme bado vijiji vinne tu

VIJIJI 73 kati ya vijiji 77 vya Wilaya ya Missenyi mkoani Kagera vimepelekewa huduma ya umeme, hivyo bado vijiji 4 tu.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa ameyasema hayo wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Kassambya, katika mikutano uliofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa, wilayani Missenyi, mkoani Kagera.

Alivitaja vijiji ambavyo havina umeme na vipo kwenye mpango wa kupelekewa nishati hiyo ni Buchurago, Katano, Kakunyu na Bugango.

Akizungmzia sekta ya mifugo ambayo imetajwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020 hadi 2025 Majaliwa alisema, Serikali ya CCM imeisimamia vizuri sekta ya mifugo ili kuhakikisha wafugaji wananufaika.

“Shilingi milioni 23 zimetumika kukarabati machinjio ya Bunazi hapa Misenyi, pia tumerahisisha uuzaji wa mazao ya mifugo kwa kufuta tozo kero 114 katika sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi na kuimarisha masoko ya mazao ya mifugo kwa kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda vya kuchakata mazao ya mifugo,” alisema Majaliwa.

Alisema serikali imepanga kuanzisha vituo vya kisasa vya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo katika mikoa 18 ambayo haina vituo, kuimarisha huduma za tiba za mifugo kwa kuhakikisha kila wilaya ina maabara, kliniki na daktari wa mifugo. Katika mkutano huo Majaliwa alimuombea kura mgombea urais kupitia CCM, John Magufuli, mgombea ubunge Jimbo la Nkenge, Dk Florent Kyombo na wagombea udiwani 13 kwenye kata za wilaya hiyo.

Majaliwa alisema Sh bilioni 3.57 zilitolewa kupitia Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (Tarura) kwa ajili ya ujenzi na matengenezo ya barabara za wilaya hiyo zikiwemo barabara za Bukwali-Kashenye-Bushango, Ngorogoro-Kyabugombe, Mabuye –Itara na Ruzinga - Mugongo.

Alizitaja barabara nyingine kuwa ni za Gera – Ishozi – Ishunju, Nyankele – Kilimilire, Mabale– Mwemage-Kyaka, NyankeleNyamilembe–Kenyana na Kituntu–Bwengabo.

Alisema mwaka 2020/21, Sh milioni 711.6 zimetolewa kupitia Tarura kwa ajili ya ujenzi na matengenezo ya barabara kwa muda maalumu.

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi