loader
Dstv Habarileo  Mobile
Majaliwa: Chagueni JPM ana hofu ya Mungu

Majaliwa: Chagueni JPM ana hofu ya Mungu

“ TANZANIA ni nchi kubwa na yenye makabila zaidi ya 120 huku wakazi wake wakikaribia milioni 60, hivyo inahitaji kiongozi mahiri na mwenye hofu ya Mungu kama alivyo, Rais John Magufuli.”

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa aliyasema hayo wakati akizungumza na wakazi wa Kata ya Ngara Mjini, kwenye mkutano uliofanyika viwanja vya Posta, wilayani Ngara, mkoani Kagera.

“Tunataka tupate kiongozi mwenye hofu ya Mungu. Tanzania inahitaji kiongozi mahiri, mzalendo, mwadilifu na mwaminifu ambaye ni lazima tujiridhishe kuwa ataweza kuongoza nchi kama alivyo Rais John Magufuli,” alisema.

Katika mkutano huo, Majaliwa ambaye pia ni Waziri Mkuu wa Tanzania, aliwaombea kura Magufuli anayegombea urais wa Tanzania kwa kipindi cha pili, mgombea ubunge Jimbo la Ngara, Ndayisaba Ruhoro na mgombea udiwani kata ya Ngara Mjini, Stanford Kennedy.

“Nimeangalia katika wote wanaotaka kupewa urais, hakuna kiongozi mwenye hizo sifa zaidi ya Dk John Magufuli. Tulimpa miaka mitano ya kuongoza nchi, amefanya mambo makubwa na nyote mmeona ama kusikia yaliyofanyika kupitia vyombo vya habari,” alisema Majaliwa.

Alisema CCM ni chama pekee kinachoweza kuwatumikia Watanzania wakiwemo wanyonge na akawaomba wananchi wawapigie kura wagombea kutoka chama hicho.

“Dk Magufuli ni kiongozi anayeweza kuiongoza nchi, ndiye kiongozi anayeweza kuunda serikali na kuisimamia ili iende kuwatumikia Watanzania mpaka wa chini kabisa kwa sababu ya uchapakazi wake.

Ikifika tarehe 28 Oktoba, nendeni mkamchague kwa kura nyingi ili aendelee kuongoza,” alisema Majaliwa. Alisema Magufuli ni kiongozi mwenye hofu ya Mungu, anayemtanguliza Mungu katika kuleta mafanikio ya taifa.

“Kwa hiyo, tunahitaji kiongozi mwenye hofu ya Mungu na ndiyo maana tulifanikiwa pia kupambana na vitu vingine vyote baada ya kumtanguliza Mungu. Kwani corona bado ipo?” aliuliza Majaliwa.

Akaongeza: “Hii ni kwa sababu ya kumwamini Mungu. Alitusihi Watanzania tufunge kwa siku tatu na tuombe kila mmoja kwa imani yake. Je hatujafanikiwa?

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi