loader
Biden atakiwa kupima Corona

Biden atakiwa kupima Corona

MAKAMU  wa  Rais  wa zamani wa Marekani na mgombea  Urais  kupitia Chama Cha Democratic,  Joe Biden ametakiwa kupima virusi vya Covid 19 vinavyosababisha ugonjwa wa Corona baada ya kuwa pamoja katika mdahalo na Rais Trump siku ya Jumanne usiku huko Cleverland.

Kwa mujibu wa mchangiaji wa masuala ya afya kutoka CNN Dr.Sanjay Gupta amesema Biden anatakiwa kupimwa mara moja kwakuwa amemkaribia mtu aliyepata virusi vya Corona.

Pamoja na hayo pia Dr. Gupta amesema ingawa Trump na mkewe Melania kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu ya nchi hiyo kuwa wako vizuri, lakini ukaribu wake na Rais huyo siku ya Jumanne umemuweka katika hatari zaidi ya kuambukizwa virusi vya Corona.

Kutokana na Rais Trump kukutwa na Virusi hivyo, Joe Biden anategemewa kupima kipimo cha Corona asubuhi hii kwa saa za huko marekani ambapo taarifa hizo zimetoka katika chanzo cha habari cha kuaminika kutoka kwa Biden.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/00cc83efec190069ba414eff6ceab9bd.jpg

Marekani na Umoja wa mataifa zimelaani vikali mauaji ...

foto
Mwandishi: Alfred Lukonge

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi