RAIS wa Marekani Donald Trump ameanza matibabu baada ya kubainika kuwa na Virusi vya Corona ambapo wamempa dawa ya majaribio inayoongeza hamu ya kula ikiambatana na kinga ya kuzuia virusi vya Remdesivir.
Hatua hii imekuja muda mchache tu baada ya yeye na mke wake Melania Trump kukutwa na virusi vya Corona.
Kwa mujibu wa mtandao wa B.B.C Daktari wa Trump, Sean Conley amesema kuwa Rais huyo alikuwa akionekana kuwa amechoka lakini hali yake inaendelea vizuri na anazidi kuimarika.