loader
Dstv Habarileo  Mobile
NCC ‘kutengeneza’ watatuzi bora wa migogoro ya kibiashara

NCC ‘kutengeneza’ watatuzi bora wa migogoro ya kibiashara

BARAZA la Ujenzi la Taifa (NCC), litatoa mafunzo ya utatuzi wa migogoro ya kibiashara kwa siku tatu Jijini Dar es Salaam, kuanzia Septemba 23 hadi 25, kwa makundi yote ya wahandisi na wataalamu wa sekta nyingine nchini, waliothibitisha ushiriki wao ndani ya muda uliopangwa.

Mtendaji Mkuu wa Baraza hilo, Dk. Matiko Samson Mturi, alisema mafunzo hayo yataendeshwa na wataalamu wabobezi wa masuala ya sheria na utatuzi wa migogoro ya kibiashara katika hoteli Holiday Inn-Posta na kuhusisha  wadau wote wa sekta ya ujenzi; wahandishi, wakadiriaji majengo, mameneja majengo na miradi, wasanifu majengo, wajenzi, wakaguzi wa viwango pamoja na wataalamu wa sekta nyingine mbalimbali wakiwemo wanasheria, maofisa bima na wanaotoka katika sekta ya usafirishaji majini.

Alisema washiriki waliotaka kuhudhuria mafunzo hayo kwa kipengele cha kutahiniwa pekee, yaani kufanya mitihani, wameruhusiwa kufanya hivyo kulingana na masharti na vigezo vilivyotolewa na NCC, ambavyo ni kulipa kwa Akaunti ya Baraza ya NMB, ada ya Sh 350,000 kwa mshiriki, tofauti na iliyopaswa kulipwa kwenye akaunti hiyo na  wanaohudhuria mafunzo yote, ambayo ni Sh 750,000.

Kwa mujibu wa Dk. Mtiru, lengo la mafunzo hayo ni kuandaa watatuzi bora wa migogoro ya kibiashara kwa njia mbalimbali zinazokubalika kisheria, ikiwemo usuluhishi, watakaozingatia sheria na haki pindi watatuapo migogoro, kutokana na misingi bora watakayofundishwa.

 “Baraza linaendesha mafunzo haya kwa mara ya 14 sasa, na yamekuwa ya mafanikio wakati wote, kutokana na mrejesho tunaoupata kupitia watatuzi wa migogoro husika, wasuluhishwa, utafiti tunaoufanya kutafuta mrejesho na njia nyingine za kupata taarifa ikwemo kupokea maoni ya wadau”, Dk Mtiru alisema.

Akifafanua kuhusu ada, alisema ni kwajili ya kulipia vifaa vitakavyotumika katia kozi hiyo, vyakula, vinywaji yakiwemo maji, pamoja na mambo yote muhimu yanayopaswa kugharamiwa katika kozi hiyo, nje ya usafiri ambao washiriki wanapaswa kujitegemea.

Vile vile, alisema, ili kufahamu jinsi wahitimu walivyoelewa walichofundishwa kwa ajili ya kukitumia, watapewa mitihani itakayogusia mambo muhimu waliyofundishwa kulingana na miongozo ya kozi husika.

Alitaja baadhi ya maeneo yatakayofundishwa kuwa ni pamoja na jinsi ya kuandaa utatuzi wa migogoro hiyo kwa njia mbalimbali, ikiwemo usuluhishi, sheria za kufuata, namna ya kuzitekeleza kufikia muafaka kusudiwa, vipengele muhimu katika utatuzi wa migogoro hiyo, gharama, jinsi ya kumpata msuluhishi, nguvu ya msuluhishi, namna ya kumaliza mgogoro ulio mahakamani na mengine. 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/f8a4d4c9438abfa04433fd3f1c09dedb.jpg

Sehemu kubwa ya ulimwengu wa biashara uli dorora kutokana na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi