loader
Dstv Habarileo  Mobile
Wakufunzi wa NCC:Epuka rushwa utatue migogoro

Wakufunzi wa NCC:Epuka rushwa utatue migogoro

WASULUHISHI wa migogoro ya kibiashara nchini na wahitimu wa mafunzo ya utatuzi wa migogoro ya kibiashara, wameonywa kuhusu rushwa na kutakiwa kuwa chachu ya usuluhishi wenye mafanikio, kwa faida ya biashara zao na uchumi wa taifa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wakitoa mafunzo kuhusu mbinu bora za kutatua migogoro ya kibiashara kwa washiriki wa mafunzo hayo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, waelimishaji wabobezi wa masuala ya usuluhishi, chini ya Mpango wa Mafunzo wa Baraza la Ujenzi la Taifa (NCC) walisema, rushwa ni kikwazo.

Waelimishaji hao; Mhandisi Samwel Msita na Wakili Rosan Mbwambo walitoa elimu hiyo kwa siku tatu mfufulizo kuanzia Jumatano iliyopita na kuwataka washiriki wa mafunzo hayo kuzingatia maadili, miongozo, sheria,kanuni na miiko ya usuluhishi, huku wakilenga kuimaliza kwa amani ili biashara zisikwame.

Mhandisi Msita aliyekuwa wa kwanza kutoa elimu hiyo alisema, "Ukiwa msuluhishi mpenda fedha utajikuta ukiuendeleza mgogoro badala ya kuumaliza, kwa sababu hutasimamia haki. Nawasihi wapenda hela kuwa makini na rushwa".

Alisema ni vyema wakati wowote wanapohitajika kutatua migogoro ya kibiashara, hata kama ni kwenye biashara zao, wasimamie haki na kuangalia namna bora ya kuzifanya pande zilizoingia kwenye mgogoro kuelewana na kuendeleza biashara.

Alisema katika biashara kuna kodi ya nchi inayopaswa kulipwa, hivyo wasuluhishi lazima wame makini kuhakikisha kupenda kwao fedha hakuwapeleki kuithamini rushwa na kuitengenezea mazingira ya ushindi zaidi ya kutatua migogoro iliyombele yao.

"Ikiwa ni kwenye eneo la manunuzi, msuluhishi zingatia sheria za manunuzi na wala usilete zakwako au kuzipindisha zilizopo kwa faida yako. Tunachokitaka ni kuona unafikiwa muafaka wenye mafanikio,"Msita alisema.

Kwa upande wake, Wakili Mbwambo alisema, siku zote msuluhishi wa mgogoro wa kibiashara anapaswa kuepuka rushwa na sababu nyingine zinazoweza kumfanya abadili kanuni, sheria na miiko ya usuluhishi, kuepuka kuupendelea upande mmoja.

Kwa mujibu wa Mbwambo, migogoro ya kibiashara inaposhindwa kumalizwa inazuia wahusika kuendelea kufanya biashara, hivyo  wasuluhishi wanapaswa kuhakikisha wanawapatanisha huku kila upande ukipata haki yake unaoidai na wala si kuendeleza mivutano inayopoteza muda.

Kutokana na maelezo yake, lengo la usuluhishi wa kibiashara ni kuwaacha walio kwenye mgogoro wa kibiashara wakiwa marafiki wenye uwezo wa kuendeleza biashara kwa amani na kuchangia kukuza uchumi wa nchi.

Mafunzo hayo ni ya 14 kuandaliwa na NCC na yalihusisha washiriki kutoka katika fani mbalimbali ikiwemo biashara, sheria, ujenzi na nyinginezo.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/93d32b2df847efd92cdad68c3021bd72.jpg

Sehemu kubwa ya ulimwengu wa biashara uli dorora kutokana na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi