loader
Macron: Iilikuwa kosa  kutojadiliana na Urusi

Macron: Iilikuwa kosa kutojadiliana na Urusi

 RAIS wa Ufaransa, Emmanuel Macron, amesema lilikuwa kosa kwa Ulaya kutojadiliana na Urusi kuhusu udhibiti wa silaha.

Aliyasema hayo katika mkutano wake wa pamoja na Waziri Mkuu wa Latvia, Krisjanis Karins.

“Makubaliano ya uzuiaji wa silaha yalihitimishwa kati ya Marekani na Urusi na hatukuwa sehemu ya makubaliano yao, lakini katika miaka 15 ya hivi karibuni mikataba hiyo imefutwa,” alisema.

Aliongeza: "Hatuna ulinzi tena. Hili hasa linahusu Mkataba wa Silaha za Nyuklia za Masafa ya Kati (INF) ambao Marekani ilijitoa. Na nini badala yake sasa? Hakuna."

Kwa mujibu wa Macron, suala hilo lingewezekana kama Ulaya ingefanya mazungumzo na Urusi juu ya masuala yanayohusiana na Ulaya na udhibiti wa silaha. 

“Naamini hili lilikuwa kosa,” alisema na kuongeza kuwa kamwe Ulaya haitapata suluhu ya suala la udhibiti wa silaha na ulinzi, endapo haitazungumza suala hilo na Urusi.

Alisema Ulaya lazima iandae mjadala na Urusi, badala ya kukabidhi suala hilo kwa Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi (Nato).

Agosti mwaka 2019 mkataba wa INF ulivunjwa kutokana na ushawishi wa Marekani, ambayo ilidai kuwa Urusi ilikataa kukubaliana na matakwa ya mahitaji ya kuondoa makombora ya kizazi kipya 9M729, ambayo Marekani na washirika wake Nato wanayaona tishio la mkataba huo.

Hata hivyo, Urusi iliyakataa matakwa hayo na kueleza kuwa makombora hayo yenye uwezo mkubwa, yapo kwa mujibu wa viwango vinavyotakiwa na mkataba huo wa INF.

Februari 2, 2019 Marekani ilionya kuwa ingejitoa kwenye mkataba huo. Ilieleza kuwa ingefanya hivyo kwa mujibu wa kanuni za mkataba huo, pale Urusi itakapokubaliana na matakwa yake, yanayohusisha kuharibiwa kwa makombora hayo ya 9M729, jambo ambalo Urusi ilikataa.

Mshauri wa Masuala ya Usalama wa Marekani, John Bolton wakati huo, alikiri kuwa uamuzi wa Marekani ulishawishiwa na ukweli kuwa China haikuwa sehemu ya mkataba wa INF.

Septemba mwaka jana, Rais wa Urusi, Vladimir Putin alizungumza na viongozi wa mataifa mbalimbali, wakiwemo wanachama wa Nato na kupendekeza kusitishwa na kupelekwa kwa makombora ya kati na masafa mafupi Ulaya na maeneo mengine, lakini Marekani nayo ilikataa mpango huo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/aa4d2be3d70295d18017ab40506f6cac.jpg

Marekani na Umoja wa mataifa zimelaani vikali mauaji ...

foto
Mwandishi: RIGA, Latvia

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi