loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Hongera Facebook kudhibiti upotoshaji uchaguzi mkuu

ZIKIWA zimebakia siku 19 kufi kia siku ya uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani Oktoba 28, mwaka huu, mtandao wa Facebook umewataka Watanzania kutoa taarifa kuhusu habari zenye viashiria vya kuchagiza uvunjifu wa amani.

Habari hizo ni zile zinazoandikwa kwenye akaunti za mtandao huo na watu mbalimbali pamoja na zinazoandikwa kwenye akaunti za uongo zinazoanzishwa kwa lengo la kuvuruga amani.

Facebook ukiwa kati ya mitandao ya kijamii yenye watumiaji wengi hapa nchini na duniani, umejipanga kukabiliana na taarifa za uchochezi zinazolenga kuhamasisha vurugu katika uchaguzi mkuu huo.

Kwa mujibu wa Meneja wa Sera wa Facebook Ukanda wa Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika, Mercy Ndegwa, kipindi cha uchaguzi mkuu mbalimbali kumekuwa na ongezeko la watumiaji wa mtandao huo hasa wanaosaka habari za siasa.

Amesema hata kwa Tanzania takwimu zinaonesha kwa mwezi uliopita na huu wa sasa kuelekea uchaguzi mkuu, kumekuwa na idadi kubwa ya watumiaji kutoka nje na ndani ya nchi na kujadili habari hasa za siasa.

Anasema Facebook imejipanga kuzifungia akaunti za mtandao huo zitakazotoa taarifa za uchochezi, uongo na za udhalilishaji katika uchaguzi wa mwaka huu, huku akiwataka Watanzania kushiriki kwa kutoa taarifa kuhusu uwapo wa akaunti hizo.

Natoa rai kwa Watanzania kushirikiana na Facebook katika kuziripoti akaunti feki zinazotoa taarifa za uongo zenye kulenga kuvuruga uchaguzi mkuu na usalama wa nchi.

Ifahamike kuwa, mitandao ya kijamii ukiwamo wa Facebook kama ukitumika vibaya unaweza kuvuruga amani na utulivu. Hii inaweza kufanyika iwapo kama watumiaji wakianza kutoa taarifa za uongo zitakazoamsha hasira za wananchi hasa kipindi ambacho matokeo ya kura yatakuwa yakitangazwa.

Wapo wagombea ambao sio tu kwa kutumia Facebook ila hata kutumia mitandao mingine kama vile Instagram na Whatsapp wanaweza kujitangazia ushindi hata kama matokeo yataonesh kushindwa.

Hatua hiyo itawarubuni wafuasi wao kiakili na kujiona kuwa wameshinda na matokeo yakitangazwa tofauti na walivyoaminishwa ndipo vurugu zinaweza kutokea.

Hivyo, ni muda sasa kuwa macho na watumiaji wabaya wa mitandao ya kijamii kwa kutoa taarifa juu ya watu wanaotumia mitandao vibaya kwa lengo la kuleta machafuko nchini.

Lakini pia ni vema kutoa taarifa kwenye mamlaka husika kama vile Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), Jeshi la Polisi au mamlaka nyinginezo ili wamiliki wa akaunti zinazotoa habari potofu waweze kukamatwa.

Ikumbukwe yapo mataifa ambayo amani yao ilivurugwa kutokana na uchochezi wa habari za uongo zilizoamsha hisia za chuki kati ya wananchi.

Matukio hayo yasipochukuliwa kwa umakini na kuzuiliwa machafuko yanaweza kutokea nchini, hivyo ni muda wa kuanza kulishughulika na watu wa namna hiyo kuanzia sasa.

Ni jambo la kufurahisha kusikia ofisi za Facebook zilizopo Nairobi, Kenya zimejipanga kuzifungia akaunti zote zitakazobainika kuchochea vurugu.

Aidha, ni jambo la faraja kuwa kuna Watanzania wengi wenye uelewa mkubwa wa masuala ya siasa wanafanya kazi katika ofisi hizo kwa lengo la kufuatilia akaunti hizo zenye lengo ovu.

Wanafuatilia wenyewe akaunti feki na zile ambazo sio feki lakini zinatoa habari chochezi na malalamiko kutoka kwa Watanzania kuhusu akaunti hizo.

Uchaguzi wa mwaka huu ni wa sita wa vyama vingi kufanyika tangu ulipofanyika wa mara ya kwanza mwaka 1995 na vyama vitakavyoshiriki uchaguzi huo ni pamoja na chama cha ADA-Tadea, Chama cha Wananchi (CUF), SAU, UPDP, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha Umma (Chauma), SAU, NCCR-Mageuzi, DP, UMD, ACT-Wazalendo, NRA, Demokrasia Makini, ADC, AAFP na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

ZIMEBAKI siku nne kufi kia siku ya Uchaguzi Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi