loader
Dstv Habarileo  Mobile
Majaliwa: Chagueni Rais madhubuti

Majaliwa: Chagueni Rais madhubuti

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amewataka wananchi ikifika Oktoba 28 mwaka huu waende kuchagua kiongozi madhubuti atakayewaletea maendeleo.

Aidha amesema kuchagua kiongozi wa kuliongoza Taifa ni muhimu na haihitaji kufanya ushabiki bali umadhubuti.

Amesema hayo jana kwa nyakati tofauti alipozungumza na wakazi wa kata za Kikunde, Tunguli na Kwekivu wilayani Kilindi, mkoani Tanga.

"Tunatafuta viongozi wa kuliongoza Taifa ambao ni Rais, wabunge na madiwani, nawaomba ifikapo Oktoba 28 mwaka huu tujitokeze kwa wingi kwenda kumchagua mgombea wa urais wa tiketi ya CCM Dk John Pombe Magufuli kwani ni kiongozi pekee atakayeweza kuwaongoza wananchi wote bila ya kujali itikadi zao vyama vyao,"alisema Majaliwa.

Alisema, Magufuli yupo kwenye uongozi si kwa majaribio, ni mtu ambaye anajua na ana uwezo wa kuwatumikia wananchi na ameuonesha mfano katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

"...Ombi hili ni kwa Watanzania wote haliangalii wewe ni wa chama gani, halina ushabiki nawaomba wote tukamchague Dk Magufuli kwa nafasi ya urais, wabunge na madiwani wa CCM nchini kote ili waweze kushirikiana kuwaletea maendeleo. Nawaomba muendelee kuwa na imani na Serikali ya CCM kwani imedhamiria kuwatumikia."alisema Majaliwa.

Alisema ni muhimu wananchi wawachague wagombea kutoka CCM kwa sababu ni chama chenye ilani inayotekelezeka tofauti na vyama vingine.

"CCM ndio jiko linaloweza kupika maendeleo, tukampigie tena kura Dk Magufuli kwa sababu mnamjua na mmesikia na kuona maendeleo aliyoyaleta nchini."alisema Majaliwa.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi