loader
Suarez asema kilichomuondoa  Barcelona

Suarez asema kilichomuondoa Barcelona

LUIS Suarez ameiambia ESPN anaamini Barcelona ilimlazimisha kuondoka klabuni hapo kwa sababu ya uhusiano wake na Lionel Messi. Suarez, 33, amejiunga na Atletico Madrid mwezi uliopita akiwa mfungaji bora namba tatu wa muda wote wa Barca akifunga mabao 198 katika miaka sita aliyokaa Camp Nou.

Kuondoka kwa mshambulijai huyo wa Uruguay kulielezwa ni kutaka kubana matumizi kwa Barca kwani kwa sasa uchumi wake hauko sawa baada ya janga la virusi vya Corona. “Kuna mkanganyiko mkubwa katika jambo hilo, kwa upande wa Barcelona,” Suarez aliliambia ESPN’s “90 Minutos” juzi.

“Ningetafuta suluhisho kama tatizo lilikuwa ni masuala ya kifedha na kama ilikuwa ni suala la kimichezo ningeelewa, haikuwa wazi kwangu kwanini walichukua maamuzi haya.”

“Nadhani walitaka kuniondoa kwa Messi, labda haikuwafurahisha kwamba nilikuwa na uhusiano mzuri na Leo. Labda hawakumtaka awe karibu na mimi kwa kiasi kile, sioni sababu yoyote ambayo ingeharibu timu.”

“Tulionekana tuko vizuri uwanjani, labda walimtaka acheze na wachezaji wengi zaidi, hiyo ni kitu kingine, sioni sababu nyingine yoyote ya kututenganisha kwa sababu tulikuwa vizuri uwanjani.” Suarez ameondoka Barca dakika za mwisho za dirisha la usajili.

Awali Messi alipambana kutaka kuondoka lakini mwishoni ikashindikana. “Walipaswa kuheshimu uamuzi wake wa kuondoka,” alisema Suarez.

Mkataba wa Messi unamalizika mwakani lakini licha ya kuamua kuondoka Barca mwezi uliopita, Suarez anaamini rafiki yake huyo ataongeza mwaka wa 20 kubaki Catalonia huku rais mpya akichaguliwa kabla ya mwishoni mwa msimu.

Malalamiko mengi ya Messi juu ya klabu hiyo mwezi uliopita ni juu ya rais wa sasa wa klabu, Josep Maria Bartomeu. “Leo anajua ana maana gani Barcelona,” alisema.

“Amepewa vitu na klabu ambavyo huwezi kudhanim ni lazima awe namba moja, awe bora na awe mwenye furaha.”

“Labda kuna uwezekano wa kucheza klabu nyingine lakini kama anajihisi vizuri na ana furaha na bodi mpya ya uongozi atataka kubaki klabuni hapo, kama rafiki yake nitakuwa na furaha kama mambo yanamuendea vizuri lakini pia hata kama atakwenda klabu nyingine.”

Kama ilivyo kwa Messi, Suarez pia amekuwa akimlaumu Bartomeu na bodi ya Barca. Anahisi alihitaji kupewa heshima zaidi.

“Imeniuliza sana na familia yangu kwa jinsi walivyonifanya,” alisema. “Haikuwa sawa kwamba kocha [Ronald Koeman] anakuja na kusema sipo kwenye hesabu zake kwamba bodi imeshasema inafanya mabadiliko makubwa.

Koeman aliniita na kuniambia sipo kwenye mipango yake lakini nilijua kitakachotokea kwa siku 10. Ni kama alithibitisha tu nilichokiona kwenye vyombo vya habari.”

“Nadhani nilistahili japo kupigiwa simu na kunieleza kwanini wanataka niondoke kabla ya kusoma kwenye vyombo vya habari.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/e768d6c3f1370b7ff80ab57af77a0ff0.jpg

Klabu ya soka ya Chelsea imefikia muafaka ...

foto
Mwandishi: MADRID, Hispania

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi