loader
Dstv Habarileo  Mobile
Tanzania yapania kuongoza uzalishaji korosho Afrika

Tanzania yapania kuongoza uzalishaji korosho Afrika

TANZANIA imejipanga kuongeza uzalishaji wa zao la korosho kutoka wastani wa tani 300,000 hadi kufi kia tani milioni moja ifi kapo mwaka 2024 na kwa kufi kia tani milioni moja Tanzania itakuwa nchi ya kwanza kwa uzalishaji wa zao hilo Barani Afrika na kuipita nchi ya Ivory Coast inaongoza sasa kwa kuwa na uzalishaji wa tani laki saba kwa msimu.

Akizungumza wakati wa mafunzo ya kilimo bora cha korosho kwa wakulima na maofisa ugani mkoani hapa yalioandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania(TARI), kituo cha Naliendele na bodi ya korosho, Mratibu wa uhahurishaji wa teknolojia TARI Naliendele,

Bakari kidunda alisema serikali imejipanga kuhakikisha inaongeza uzalishaji na kufikia tani milioni moja kwa msimu kutokana na mpango wa kuongeza maeneo ya uzalishaji wa korosho kwa mikoa mingine mipya na utafiti unaonesha zaidi ya mikoa 17 inaweza kustawi zao la korosho hapa nchini.

Kidunda alisema kuwa pamoja na kuongeza maeneo ya uzalishaji wa korosho utoaji wa mafunzo ya kilimo bora cha korosho pia ni muhimu katika kuongeza uzalishaji wa zao hilo katika maeneo hayo, hivyo TARI Naliendele na bodi ya Korosho Tanzania wanaendesha mafunzo ya kilimo bora cha zao hilo kwa maofisa ugani na wakulima ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo.

Alisema waliona watoe mafunzo kwa mikoa mipya ambayo imeanza kulima zao hilo baada ya kituo hicho cha utafiti TARI Naliendele kufanya utafiti na kubaini kuwa ardhi yake inafaa kwa ulimaji wa zao hilo lengo likiwa ni kuongeza tija na uzalishaji.

Alisema kuwa tani zaidi ya laki tatu zilizozalishwa mwaka 2017/18 ilikuwa inalimwa na mikoa mitano pekee na kuitaja kuwa ni Lindi, Mtwara, Ruvuma, Pwani na Tanga na kuongeza kuwa mikoa hiyo mipya uzalishaji utaongezeka na kufikia tani hizo na hivyo kuifanya nchi kuongoza katika uzalishaji wa zao hilo Barani Afrika.

Aidha aliitaja baadhi ya Mikoa mipya ambayo imeanza kulima zao hilo kuwa ni pamoja na Iringa, Mbeya, Rukwa, Katavi, Songwe, Kigoma, Morogoro, Singida, Kilimanjaro, Dodoma,Tanga, Pwani, Shinyanga, Njombe na Simiyu. mtafiti kutoka kituo cha Utafiti wa kilimo Tari Naliendele kitengo Cha Agronomia ya Mkorosho, Masana Joseph alisema kuwa katika maeneo mapya kuna changamoto ya uandaaji wa mashamba na kuwa wanatafuta dawa ya kuua magugu kwa ajili ya kukausha visiki badala ya kuvichimba na kuvitoa.

Aliitaja changamoto nyingine kuwa ni namna ya utunzaji wa miche ya mikorosho mashambani na kuongeza kuwa wengi wamekua wanapanda na kuiacha bila kuifanyia usafi jambo ambalo linachangia moto unapoingia unachoma mikorosho yote kutokana na uchafu wa shamba.

Joseph alisema kuwa wakulima wanapaswa kutambua kuwa visiki vyote vinapaswa kutolewa ikiwa ni pamoja kuzingatia upandaji wa nafasi kama walivyoelekezwa na wataalamu.

Mkulima wa zao hilo wilayani Sumbawanga, Charles Kaziulaya alisema kuwa alipata hamasa kutoka kwa mtaalamu wa kilimo wilayani hapo na kuwa baada ya kupata hamasa hiyo aliamua aanze kulima korosho na kwamba alianza na ekari 10.

Mkurugenzi Mkuu wa taasisi ya utafiti wa Kilimo Tanzania TARI Dk Geoffrey Mkamilo alisema kuwa kupitia elimu ambayo wakulima katika mikoa mipya wanaipata itasaidia kuongeza tija na uzalishaji katika zao hilo na hivyo kufikia malengo ya serikali ya kufikia uzalishaji wa tani milioni moja ifikapo 2024.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/ae6ad1f381d31c4b2cd5cbbe8ca42f08.jpg

Sehemu kubwa ya ulimwengu wa biashara uli dorora kutokana na ...

foto
Mwandishi: Agnes Haule, Rukwa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi