loader
Majaliwa awataka Zanzibar kumchagua Magufuli

Majaliwa awataka Zanzibar kumchagua Magufuli

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa Zanzibar wamchague John  Magufuli kwa kuwa ni mgombea pekee mwenye uwezo wa kudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Aliyasema hayo wakati akizungumza na wakazi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, katika mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa Kairo, Kiwengwa, wilaya ya Kaskazini B.

"Nawaletea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amefanya makubwa kwenye uongozi wake uliopita. Hata kwenye wizara alizowahi kuongoza, pia amefanya makubwa. Ndiye mgombea pekee mweye uwezo wa kutuunganisha Wazanzibari na Watanzania Bara," alisema Majaliwa.

Alisema, kuna baadhi ya wagombea wanaotangaza kuwa wakichaguliwa watauvunja muungano hivyo ametaka wawaepuke.

 

Majaliwa alisema, kazi ya urais si ya mchezo na inataka mtu makini, kwa hiyo akawaomba wananchi wamchangue mtu mwenye uwezo wa kupambana na wala rushwa.

 

Majaliwa yuko Zanzibar kuwaombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM,  Magufuli, mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk Hussein Mwinyi, wagombea ubunge wa majimboi, wawakilishi na wagombea udiwani.

 

Wakati akimuombea kura Dk Mwinyi, Majaliwa alisema, CCM ina benki ya kutosha ya makada wenye uwezo wa kuongoza.

 

"Chama Cha Mapinduzi kina nafasi nyingi za uongozi, na katika nafasi hii ya kuongoza Zanzibar, tumemleta Dk Hussein Mwinyi."alisema Majaliwa.

 

Alisema, Rais Dk Ali Mohammed Shein amefanya mengi mazuri na yaliyobaki yatakamilishwa na Dk Mwinyi.

 "Masuala yote ya kipaumbele yamewekwa kwenye ilani ya uchaguzi ya yenye kurasa 303. Pia kitabu hiki kimesambazwa hadi kwenye shehia zenu. Kitafuteni mkisome ili muone mambo yaliyopangwa kufanyika kwa ajili ya Zanzibar."alisema na kuongeza;

 

"Maendeleo ya mifugo yamo humu, maendeleo ya uvuvi yamo humu, maendeleo ya ajira yamo, kuwezesha sekta binafsi yamo humu, kuwezesha viwanda yamo humu, kuwezesha wajasiriamali wadogo, wa kati na wakubwa nayo pia yamo humu," ameeleza.

 

Mapema, Dk  Mwinyi alisema serikali yake itaimarisha uvuvi wa bahari kuu pamoja na bandari za uvuvi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa viwanda vya kusindika samaki ili kuongeza ajira na masoko kwa bidhaa za baharini.

 

Alisema ataimarisha ufugaji wa samaki ikiwa ni njia mojawapo kuu ya kulinda mazingira. "Nitasimamia hilo la ufungaji wa samaki hasa kwenye maeneo ya mikoko kwa sababu tutakuwa pia tunalinda mazingira yetu," alisema Dk Mwinyi.

 

Alisema, atashughulikia tatizo la mmomonyoko wa maadili na hasa tatizo la matumizi ya dawa za kulevya na udhalilishaji kwa wanawake na watoto.

 

Dk Mwinyi alitumia fursa hiyo kumuombea kura Dk Magufuli, wabunge, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na madiwani wa CCM.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/7fb5057d7a22cbb8fb52e984e9def818.jpg

RAIS Samia Suluhu Hassan amehutubia taifa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

1 Comments

  • avatar
    Loshiye Mollel
    14/10/2020

    Nikweli nchi hii rais makufuli yatosha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi