loader
Cedric Kaze rasmi kuonoa Yanga mpaka 2022

Cedric Kaze rasmi kuonoa Yanga mpaka 2022

UONGOZI wa  Yanga  umemtambulisha rasmi kocha Cedric Kaze   na kumpa mkataba wa miaka miwili.

Yanga imemtambulisha rasmi leo ambapo mkataba wake utamalizika mwaka 20222.

Akuzungumza jijini Dar es Salaam leo, Kaze amesema kitu cha kwanza ambacho atakipa kipaumbele ni kuhakikisha anawapa wachezaji wazingira mazuri ambayo yatawawezesha kuwa huru kucheza na kufanya vizuri.

“Maneo mengi sio yanayofanya kazi uwanjani, acha tungoje, tutumike sana,  kuna watu wanatamani kuona vile tutaweza,” amesema Kaze na kuongeza

“Kitu ninachokipa kipaumbe ni wachezaji ambao watafanya kazi, nitakachofanya ni kuwandalia mazingira mazuri ambayo yatawawezesha kufanya kazi ili kutoa matokeo mazuri na kuwapa furaha wana yanga,” amesema

Kaze ametua ametua nchini usiku wa kuamkialeo akitokea Canada na  kupokelewa na viongozi na baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo waliojitokeza katika uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar es Salaam.

 Aidha Kaze amesema anaimani atafanya kazi vizuri na klabu hiyo kwani ni klabu kubwa na yenye mashabiki wengi barani Afrika na kuwataka mashabiki kuiunga mkono timu hiyo ili iweze kupata mafanikio.

“Naweza kuwaambia mashabiki wetu wajiandae kabisa kuisapoti timu tushirikiane najua kama tutafanya vitu vikubwa”, amesema Kaze.

Kocha huyo wa zamani wa vilabu ya  Vital’O na Atletico FC anakuja kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Mserbia Zlatko Krmpotic aliyevunja mkataba na klabu hiyo mapema mwezi huu baada ya mchezo dhidi ya Coastal Union uliomalizika kwa Yanga kushinda Goli tatu  kwa sifuri.

 Licha ya kutua leo, Klabu ya Yanga ilimalizana na Mburundi Cerdric Kanze mapema kabisa lakini baadae alishindwa kuwasili nchini. Ndipo ikawalazimu kumpata Mserbia Zlatko Krmpotic ili aweze kuchukua nafasi hiyo.

Cedric Kaze ni kocha Raia wa Burundi mwenye leseni ya shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika (CUF) pamoja na shirikisho la soka nchini Ujerumani (DFB). 

Yanga ipo nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi ikiwa na point 13 na kucheza mechi 5.

Cedric Kanze ambaye ni kocha bora nchini Burundi kwa msimu wa mwaka 2011/2012 atakuwa na kibarua cha kukiongoza kikosi cha wananchi katika mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu soka Tanzania Bara siku ya Octoba 22  dhidi ya Polisi Tanzania.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/71a68f3d42f013c47a2f5765f031119d.jpg

CHAMA cha Makocha wa Ligi Kuu England ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi