loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tujitokeze kwa wingi mikutano ya kampeni

I DADI ya siku za kupiga kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020, inazidi kupungua. Watanzania wanazidi kutamani kusikia wagombea wa nafasi mbalimbali wana sera gani na wamejipanga vipi kuwaongoza kuelekea maendeleo wanayoyataka.

Kimsingi, katika mikutano ya kampeni, ndipo wananchi wanapopata fursa za kuwasikia na kuwajua wagombea sambamba na kuwachuja wanaosema wasiyoweza kuyatenda, na wanaosema wanayoweza na wanayotaka kuyafanya kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania.

Ndiyo maana nionavyo mimi, mikutano ya kampeni siyo mahali pa kukosa kwa mtu asiye na kikwazo kikubwa, bali sehemu muhimu kufuatilia ili kujua wagombea ambao ni ‘mchele’, na wagombea ambao ni ‘pumba’ maana kizuri chajiuza, kibaya chajitembeza.

Kwa msingi huo, wagombea na wanasiasa au wafuasi wao katika vyama mbalimbali, wafuate sheria, kanuni, miongozo na taratibu zilizopo kwa kuzingatia muda, maeneo na maneno wanayoyatoa ili wasijipeleke kwenye mdomo wa mamba ili waadhibiwe maana mbaazi akikosa maua, husingizia jua.

Kwa maoni yangu, mgombea anayekiuka taratibu au sheria kwa makusudi ili aadhibiwe, ni wazi hana sera wala hoja hivyo, anatafuta kisingizio ali apumzike na kutafuta namna ya kuongopa.

Ni kwa msingi huo, wananchi nao wanao wajibu kuhudhuria mikutano ya kampeni kistaarabu na kiungwana bila kuzua chokochoko dhidi ya mgombea au chama chochote.

Mikutano ya kampeni siyo mahali pa wananchi kupiga kura kuwakataa hapo hao wanaoona hawafai, bali sehemu ya kuwajua wagombea na vyama vyao.

Kwangu mimi, mikutano hiyo ihudhuriwe na kufanyika kwa busara; wagombea na wafuasi wao waongozwe na busara kwa kampeni za kistaarabu, na wananchi wasikilize na kuchuja mchele na pumba kistaarabu ili Oktoba 28, 2020 ikiwadia, wafanyae uamuzi makini kwa kuchagua wagombea walio ‘safi’. Kwa siku tisa zilizobaki, tujitokeze katika mikutano ya kampeni.

ZIMEBAKI siku nne kufi kia siku ya Uchaguzi Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Joseph Sabinus

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi