loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Shein awapa pole wanachama CCM waliovamiwa na kupigwa

RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein jana alikwenda katika Hospitali ya Micheweni kwa ajili ya kuwapa pole wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliovamiwa na kupigwa katika Kijiji cha Kwale, Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Alifika hospitalini hapo jana asubuhi na kupokewa na viongozi mbalimbali wa mkoa na wilaya hiyo pamoja na madaktari wa hospitali hiyo ya Micheweni wakiongozwa na daktari wa hospitali hiyo, Dk Mbwana Shoka Salum.

Akitoa maelezo ya wagonjwa hao, Dk Salum alisema kuwa wagonjwa hao walipokewa juzi usiku wakiwa na majeraha makubwa na mmoja kati ya hao, Khatib Said Khatib (43) alikuwa katika hali mbaya.

Kwa mujibu wa uongozi wa Jeshi la Polisi walieleza kuwa tukio hilo limetokea wakati wafuasi wa chama kimoja cha upinzani walipokuwa wakirudi katika mkutano wao wa kampeni Chamboni, wilaya ya Micheweni na kupita katika kijiji cha Kwale na ndipo walipowashambulia kwa kuwapiga wanachama hao wa CCM.

Miongoni mwa majeruhi wa tukio hilo ni Khamis Hamad Haji (70), Yassir Hemed Abdi (18), Hassan Khamis Hamad(33), Juma khatib Rajab(34), Abdalla Khamis Mbarouk (30), Khatib Said Khatib (43) na Raya Khamis Hamad (24).

Kwa mujibu wa maelezo ya Dk Salum, majeruhi Khatib Said Khatib (43) ndiye aliyekuwa na hali mbaya wakati alipofika hospitalini hapo kutokana na majeraha ya kupigwa kisu cha tumbo na mbavu.

Aliongeza kuwa majeruhi wengine walipata majeraha yakiwemo kupigwa na vitu vyenye ncha kali sehemu ya kichwa, tumbo na miguu wakati Raya Khamis Hamad (24) ambaye ni mjamzito mtoto wa Khatib Said Khatib (43) alipigwa mateke ya tumbo wakati akimtetea baba yake.

Rais Shein akiwapa pole majeruhi hao aliwaeleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko pamoja na wao na itahakikisha inawakamata wahusika wote na baadaye kuwachukulia hatua husika za kisheria.

Aliwaeleza wananchi hao kuwa serikali itahakikisha inaendelea kuzilinda familia zao, makazi yao na pamoja na mali zao zote.

Dk Salum alitoa shukurani kwa serikali kwa kuiimarisha hospitali hiyo na kueleza kuwa wananchi wa Micheweni na vitongoji vyake wanaridhika na huduma zinazotolewa na hospitali hiyo zikiwemo huduma za upasuaji na pia alipongeza ushirikiano uliooneshwa na viongozi wa mkoa, wilaya na wengineo katika kuwasaida wananchi hao waliopigwa muda wote wakiwa hospitalini hapo.

Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mohammed Hassan Haji alimueleza Rais Shein kuwa tayari watuhumiwa 57 wa tukio hilo wameshakamatwa na bado polisi inaendelea kuwasaka zaidi wahusika wengine.

Raya Khamis Hamad akimueleza Rais Shein maswahiba yaliyomkuta na kupelekea kupigwa mateke ya tumbo, alisema kuwa ipo haja kwa vyama vya siasa kuheshimiana kwani si jambo la busara kufanyiana matukio kama hayo hasa ikizingatiwa kwamba wao wana chama chao cha CCM na hawamchokozi mtu lakini wao wanachokozwa.

WAZAZI nchini wameaswa kuisaidia serikali kutatua baadhi ya changamoto zinazoikabili ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Pemba

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi