loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

NEC yaonya wasimamizi wa uchaguzi

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema haitasita kumchukulia hatua msimamizi wa uchaguzi atakayekuwa chanzo cha malalamiko au atakayeharibu uchaguzi katika wilaya au jimbo analosimamia.

Mwenyekiti wa kikao cha mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi kutoka mikoa sita, Jaji mstaafu, Mary Longway alisema tume haitakuwa na msamaha kwa msimamizi atakayevuruga uchaguzi.

Kikao hicho kilichohusisha mikoa ya Pwani, Morogoro, Dodoma, Singida, Shinyanga na Tabora, kilifanyika mjini hapa.

Longway ambaye ni Mjumbe wa NEC alisema msimamizi atakayechangia kuleta malalamiko yatakayosababisha uchaguzi kupingwa mahakamani na mahakama ikafuta matokeo, akasababisha serikali kuingia gharama kufanyika uchaguzi wa mdogo au wa marudio, atatakiwa kulipa fidia ya gharama hizo.

“Msimamizi atakayeshindwa kusimamia vizuri uchaguzi na kusababisha uchaguzi katika eneo hilo kurudiwa na hivyo kuitia hasara serikali kwa kufanya uchaguzi wa marudio, atatakiwa kulipa fidia ya gharama hizo,” alisema.

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Uchaguzi, Leonard Tumuo alisema, wasimamizi wa uchaguzi wanatakiwa kuhakiki vifaa vilivyosambazwa na tume kama vimefika vyote zikiwamo karatasi na nukta nundu kuhakikisha vinatosheleza na kama kuna upungufu watoe taarifa mapema.

Tumuo ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala wa NEC alisema, licha ya kukagua vifaa hivyo, pia wanatakiwa kukagua vituo vya kupigia kura.

Alisema wananchi wakishapiga kura Oktoba 28, wanatakiwa kuondoka vituoni na wasimamizi bila kupoteza muda wanatakiwa kujumlisha kura kuepusha vurugu zinazoibuka kutokana na kuchelewesha matokeo.

Alisema tume ina hakika wasimamizi wa uchaguzi wamechagua watendaji wa vituo wenye weledi ambao watatakiwa kufungua vituo saa 1 asubuhi na wao wanatakiwa kuwahi kabla kujiandaa kabla ya kufungua vituo muda huo uliopangwa.

Wasimamizi wa uchaguzi wanatakiwa kuhakikisha kwamba wanawasiliana na viongozi wa vyama vya siasa kuwasilisha majina ya mawakala mapema ili kuwaapisha katani ifikapo Oktoba 21, mwaka huu.

Akizungumza katika kikao hicho, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Iramba Mashariki, Geofrey Sanga alisema ameshafanya maandalizi na yamefikia asilimia 95.

Msimaizi wa uchaguzi Jimbo la Iramba Mashariki, Charles Fusi alisema wameshapokea vifaa vyote na wameshajenga vituo kwa ajili ya kupigia kura.

Fusi alisema wamejiandaa kusimamia vizuri uchaguzi huo na kuhakikisha kwamba haki inatendeka na wananchi wanatumia haki yao kupiga kura katika kuchagua viongozi wao.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu kutakuwa na vituo vya kupigia kura 81,567 na wapigakura 29,188,387 katika majimbo mbalimbali nchini

ILANI ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi