loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kikwete: Magufuli ni nahodha hodari, jasiri

RAIS mstaafu, Jakaya Kikwete ametaka Watanzania kukichagua Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiendelee kuongoza huku akimtaja mgombea wake wa urais, Rais John Magufuli ni nahodha hodari, makini, jasiri na shupavu aliyetekeleza ilaji kwa kiwango cha hali ya juu.

Akihimiza kuzingatia ‘mafiga matatu’ kwa maana ya kuchagua rais, wabunge, wawakilishi na madiwani kutoka CCM, Kikwete alitaja sababu za kuchagua chama hicho pamoja na Magufuli miongoni mwake ikiwa ni amani ambayo alisema mataifa mengi yanaoionea wivu Tanzania.

Kikwete alisema hayo Dar es Salaam jana alipohutubia mkutano wa kampeni katika viwanja vya Zakhem, Mbagala. “Magufuli amejipambanua kuwa nahodha hodari, makini, jasiri na shupavu.

Ameongoza utekelezaji wa ilani kwa kiwango cha hali ya juu sana. Zaidi ya asilimia 80 imetekelezwa na pale palipobaki si kwa uzembe ni kwa sababu ipo kazi inayoendelea, haikumalizika 2020 lakini mkimpa nafasi tena atamaliza,” alisema.

Alisema Magufuli akichaguliwa, atamalizia na kutekeleza yaliyomo katika ilani mpya ya 2020-2025. “Tuendelee kukipa Chama Cha Mapinduzi chenye ilani ya uhakika. Ilani ya sasa ina mambo hujapata kuona.

Tanzania itakuwa ya aina yake kabisa. Tanzania itakuwa mahali pazuri. “ Kikwete alisema anachaguliwa kiongozi atakayetatua changamo hivyo Watanzania hawapaswi kucheza kamali vinginevyo, wakikosea watajuta.

Akimwelezea Magufuli, alisema mwaka 2015, moja ya ajenda kubwa ilikuwa ni kupambana na rushwa na ndicho kilikuwa kilio kikubwa cha watanzania hali iliyosababisha chama kutafuta mgombea asiye na makandokando ya rushwa.

“Na kwa chaguo letu la Magufuli hatukukosea kwa maana ya kupambana na rushwa.,” alisema. Kikwete alisema kutokana na Rais Magufuli kupambana ipasavyo na rushwa, katika kipindi hiki cha kampeni hajasikia mgombea anayezungumzia matatizo ya rushwa.

“Na atakayezungumza kama ajenda atakuwa ameishiwa. Huyo ndiye John Magufuli.”

Kwa nini CCM?

Akieleza sababu za kuchagua CCM, Kikwete alisema chama kina sera sera nzuri zenye kujali, kuendeleza na kudumisha maslahi ya kisiasa, kiuchumi kijamii kiutamaduni na kiusalama wa nchi na watu wake.

Alisema, “Hakuna chama kingine kinachofanana na CCM, mimi sikijui kwa ufasaha wa sera na sera zenyewe hakuna wa kuishinda wala wa kuikaribia.”

Alisema sera nzuri zimeliunganisha taifa na kujenga umoja wa watu wa rangi, dini, makabila na wafuasi wa vyama tofauti. “Na wengi wanatuonea wivu. Wanatuuliza kwa nini wenzetu mmefanyaje? Siri yenu ni nini? Nawaambia hivi usione vinaelea vimeundwa …na muundaji ni sera safi za chama cha mapnduzi ndizo zimetujengea taifa hili lenye umoja.

“ Alitaja sababu nyingine ya kuchagua tena CCM kuongoza nchi ni kutokana na kutekeleza ilani za uchaguzi zinazotambua changamoto zinazokabili wananchi. Alisema ilani inazungumzia masuala yanayohusu watanzanaia katika nyanja mbalimblia ya maisha yao.

“Mkiwa na nahodha asiye makini itatekelezwa ndivyo sivyo,” alisema.

Kikwete alisema serikali imetekeleza kazi nzuri imefanyika katika nyanja zote za maisha ya Watanzania hususani afya, elimu, huduma za maji na ujenzi wa miundombinu ya barabara na viwanja vya ndege.

Alishangaa wanaohoji hatua ya kiwanja cha ndege kujengwa Chato mkoani Geita wakati karibu mikoa yote ina viwanja na uliokuwa umebaki ni Geita.

“Unajua mambo haya unatakiwa uwe na ngozi ngumu. Wakati huo tunajenga barabara ya Bagamoyo-Msata, bungeni kulikuwa na vurumai sijapata kuona… rais anajenga barabara ya kwao,” alisema na kushangaa wanaobeza barabara za juu zilizojengwa Dar es Salaam kukabili msongamano wa magari

ILANI ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi