loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Takukuru Kibaha waokoa milioni 241/-

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) katika Mkoa wa Pwani imeokoa mali na fedha taslimu Sh milioni 243.1 katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

Mkuu wa Takukuru mkoani Pwani, Suzana Raymond, alisema fedha hizo zimeokolewa katika kipindi cha robo mwaka kuanzia Julai hadi Septemba mwaka huu kutokana na baadhi ya watendaji wa serikali waliojipatia fedha hizo kwa udanganyifu kinyume cha sheria.

“Moja ya mafanikio ni kurejesha fedha kwenye akaunti ya Halmashauri ya Chalinze kiasi cha Sh milioni 6.4 zilizotokana na ukiukwaji wa taratibu za mikopo inayotolewa kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu uliofanywa na kikundi cha Miono Saccos cha Kata ya Miono baada ya kupokea kiasi cha Sh milioni 9.1 kutoka halmahauri,” alisema Raymond.

Alisema walibaini kuwa, viongozi wa kikundi hicho walipokea mkopo huo usio na riba na kukopesha wafanyabiahara pasipo kuwajulisha wanakikundi wengine kinyume cha masharti ya mkopo huo unaotolewa kwa mujibu wa Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, Sura 290, Kifungu cha 37 (a) (4).

“Tulifanikiwa pia kurejesha Sh milioni 1.3 katika akaunti ya Kijiji cha Msoga, Kata ya Msoga, Halmashauri ya Chalinze katika Wilaya ya Bagamoyo.

Fedha hizi zilitokana na mapato yatokanayo na madini ya ujenzi, zilifanyiwa ubadhirifu na aliyekuwa Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Msoga,” alisema Raymond.

Alisema mtendaji huyo alipokea kiasi hicho cha fedha kwa nyakati tofauti kutoka kwa mkusanya ushuru wa kijiji hicho na kuzitumia kwa matumizi yake binafsi ambapo baada ya kuhojiwa alikubali kukabidhi fedha hizo na kuomba kuzirejesha kwenye akaunti ya kijiji.

“Tulifanikia kurejesha Sh 5,000,000 kutoka kampuni ya Mafubilo ikiwa ni sehemu ya deni kwa wakulima wa korosho anaounda umoja wa UVUKI Wilaya ya Kibaha na tumefanikia kusaidia wafanyakazi wa kampuni ya ulinzi kulipwa viwanja badala ya fedha walizokuwa wakidai kampuni ya PRC Associate security T Ltd ya Kibaha baada ya kushindwa kuwalipa mishahara kwa kipindi cha miaka mitatu kiasi cha Sh milioni 23,” alisema.

Raymond alisema mmiliki wa kampuni hiyo alipofuatwa na Takukuru alionesha ushirikiano na kuamua kuwalipa viwanja badala ya fedha chini ya usimamizi wa serikali ya mtaa na watumishi hao kuridhika na hatua hiyo kwani walihangaika kutafuta haki yao sehemu mbalimbali bila ya mafanikio.

Kwa upande wa Wilaya ya Mafia alifanikiwa kuokoa Sh milioni 4.2 zilizokusudiwa kuchepushwa na baadhi ya watumishi na mawakala wa halmashauri wenye dhamana ya kukusanya ushuru kwa kutumia mashine za kieletroniki na pia, Sh milioni 4.9 zilirejeshwa kwenye akaunti ya Chama Cha Ushirika wa korosho na nazi wilayani humo.

“Viongozi hao wa chama kwa sasa wamesimamishwa ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili,” alisema Raymond. Alisema katika Ofisi ya Wilaya ya Kibiti, wameokoa mabati 168 geji 28 yenye thamani ya Sh milioni 4.7 yaliyotakiwa kuezekwa kwenye madarasa ya shule shikizi ya msingi ya Nyambangala kwenye kata ya Dimani.

“Hata hivyo msimamizi mkuu wa mradi huo mkuu wa shule alishirikiana na makandarasi na kuezeka kwa kutumia mabati geji tatu tofauti na mkataba ulivyoonesha, hivyo ikabidi yaondolewe na kuezekwa mabati yaliyoandikaa kwenye mkataba,” alisema Raymond.

Aidha, waliokoa Sh milioni 64.9 zilizochepushwa na wanunuzi wa korosho; Sh milioni 50 na Sh milioni 14.9 zilichepushwa na viongozi wa Amcos na baada ya fedha kurejeshwa, walilipa wakulima waliokuwa wanadai katika vyama vya Juhudi, Mambao na Ruaruke.

“Katika Wilaya ya Rufiji, tuluiokoa Sh milioni 2.5 kutokana na tozo za kodi kutoka kwa mfanyabiahara mmoja aliyekiuka taratibu za uvunaji wa mazao ya misitu kwa kuvuna magogo ya miti ya mkuruti katika maeneo yasiyoruhusiwa.

Aidha, tuliokoa Sh milioni 1.2 zilichotokana na ukiukwaji wa taratibu uliofanywa na maofisa wa halmashauri ya wilaya kwa kufanya ukadiriaji mdogo wa ujazo wa magogo yaliyokuwa yanapigwa mnada katika Kijiji cha Nyamwage,”alisema Raymond.

Aliongeza kuwa, waliokoa Sh 900,000 kutokana na malipo hewa ya mauzo ya korosho yaliyolipwa kwa mfanyabiahara mmoja kinyume cha utaratibu kwani hakustahili kupata malipo hayo, hivyo aliamuru mfanyabiahara huyo kurejesha fedha hizo pia wakarejesha Sh milioni 1.2 ambazo maofisa ardhi wa wilaya wailijipatia kwa njia zisizo halali kwa kuuza viwanja bila ya mwajiri wao kujua.

Raymond alisema pia walimsaidia mkazi wa Mtaa wa Bomani katika Wilaya ya Kisarawe, Khadija Bani, kulipwa Sh milioni 12.5 ikiwa ni sehemu ya Sh milioni 26 alizotakiwa kulipwa zikiwa fidia ya mazao katika shamba lake lililochukuliwa na kampuni ya Rak Kaolin Co Ltd mwaka 2016.

Kwa mujibu wa Raymond, walirejesha Sh 930,000 kwenye akaunti ya halmashauri kutoka kwa Ofisa Mtendaji wa Kata ya Vikindu, Shaban Mponda alizopokea kutoka kwa watendaji wa vijiji kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya kata, lakini akazifanyia ubadhirifu.

“Tulifanikiwa kufufua mradi wa maji katika Shule ya Sekondari Pazuo, mradi uliokufa tangu mwaka 2017 baada ya mkandarasi SEBA Contruction Co Ltd kutumia paneli kwa ajili ya umeme wa jua na pampu ya maji ambavyo havikuwa na ubora na mradi huo kushindwa kutoa maji.

Baada ya Takukuru kuingilia kati, sasa maji yanatoka na alitumia Sh milioni 32.2,” alisema Raymon

ILANI ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka ...

foto
Mwandishi: John Gagarini, Kibaha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi