loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Lissu aonywa kubeza maendeleo ya wazi

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza kimemuonya mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Tundu Lissu kutoyabeza maendeleo yaliyoletwa na Rais John Magufuli ambaye katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake, amefanya mambo makubwa ya maendeleo ya kujivunia hapa nchini.

Kauli ilitolewa kisiwani Ukara na Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya CCM mkoa wa Mwanza jana, Jamal Babu ambaye alisema kutokana na rekodi kubwa ya utendaji kazi iliyofanywa na Rais Magufuli, njia ya kwenda Ikulu iko wazi na kwamba CCM itashinda uchaguzi huo kwa kishindo.

Sanjari na kuwaomba wakazi wa Ukerewe kumpatia kura za ushindi Magufuli, alisema rais huyo amefanya mambo makubwa ikiwemo ununuzi wa vivuko katika maeneo mbalimbali ya nchi na ujenzi na ukarabati wa meli tatu katika ziwa Victoria.

Alisema madai yaliyotolewa na mgombea huyo wa Chadema ya kutoruhusiwa kutumia moja ya feri zinazofanya huduma ya usafirishaji kwenda wilayani Ukerewe wiki iliyopita, yanayoonesha jinsi Lissu amekuwa akibeza mambo makubwa ya maendeleo yanayofanywa na serikali kwa ujenzi wa kile alichokibeza cha vitu badala ya maendeleo ya watu.

 “Yeye amesikika akibeza maendeleo ya vitu yanayofanywa na serikali, iweje leo aje kuomba kutumia kivuko kilichotengenezwa na serikali ya CCM, aende Ubelgiji akaifuate huko feri, maana amekuwa akibeza maendeleo ya vitu hayana tija,” alisema.

Aliishukuru serikali kwa ujenzi wa kivuko hicho, hatua inayoonesha jinsi imetekeleza vyema ilani ya CCM na kwamba sasa kinakwenda kutatua changamoto ya usafiri wa majini kwa wakazi wa Ukara na Ukerewe kwa ujumla.

 

MKURUGENZI Mkuu wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS), ...

foto
Mwandishi: Nashon Kennedy, Mwanza

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi