loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Mbunge aahidi kutumia vipaji kuleta maendeleo

MGOMBEA ubunge Jimbo la Ubungo kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Pamba Mkongo amesema akichaguliwa kuwa mbunge atatumia vipaji vya watu walivyojaliwa na Mungu kuwaletea maendeleo.

Alisema chama hicho kitalea vipaji hivyo kwa kuviongezea uwezo kuwasaidia kuwaongezea kipato chao na kukuza uchumi.

Alisema pindi akichaguliwa atapeleka hoja binafsi bungeni ili ibadilishwe sera ya bima ya afya iwe bure.

Alisema hayo jana alipokuwa kwenye viwanja vya Kagera kwenye kampeni za kuomba wananchi wa jimbo hilo kumchagua kwa nafasi hiyo.

Alisema atapeleka hoja binafsi ili ibadilishwe sera ya afya iwe bure au ipunguzwe ili mwananchi wa chini aweze kuchangia kiwango cha chini.

"Tumeona mtu akifa hospitalini maiti imekuwa kama biashara, tutalisemea bungeni ili tozo ya kuhifahi mwili iweze kupunguzwa na wananchi wa chini waweze kuimudu,"alisema.

Pia alisema watatengeneza ajira za watu, watasimamia mikopo ya pikipiki kwa vijana ambapo watapita kwenye vikundi vya bodaboda ambapo ofisi ya mbunge itakuwa mdhamini.

Alisema vijana wa bodaboda wanapewa mikataba na watu wenye fedha wanapokwenda benki kukopa pikipiki wanachukua kwa Sh milioni mbili lakini anapoingia mkataba na dereva wa bodaboda anaambiwa atoe zaidi ya Sh milioni nne.

Naye mgombea udiwani Kata ya Makurumla wa chama hicho, Omary Kombo maarufu Kijiko alisema atahakikisha mazingira ya eneo hilo yanakuwa safi na salama kwa kuzoa taka kwa wakati.

Kombo alisema ataendelea kuboresha huduma ambazo bado hazijaanza kupatikana katika kituo cha afya cha Makurumla.

WENYE ligi yao wameanza kurejea kwenye nafasi zao. ...

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi