loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

CCM yalalamika ZEC kushambuliwa wafuasi wake

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimewasilisha malalamiko kwenye Kamati ya Maadili ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kupinga kushambuliwa wafuasi wake walipokuwa kwenye mikutano ya kampeni.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk Abdallah Juma Sadalla alisema hayo katika Hospitali ya Micheweni alipwatembelea wafuasi saba wa CCM waliojeruhiwa kwa kushambuliwa kwa mawe na silaha nyingine za jadi.

Dk Sadalla alisema, matukio hayo hayakubaliki kwa kuwa yana lengo la kuwatisha wafuasi wa CCM ili washindwe kutumia haki yao ya kidemokrasia kupiga kura.

“Chama Cha Mapinduzi (CCM) tumeandika barua ya malalamiko kwa kamati ya maadili ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kuhusu matukio ya vitendo vinavyofanyika na wafuasi wa vyama vya siasa kwa kuwashambuliya wafuasi wa CCM...tumesikitishwa na matukio mawili yaliyojitokeza hivi sasa”alisema.

Sadalla alisema siasa za chuki na uhasama zimepitwa na wakati na kuna baadhi ya vyama vya siasa vinadhani wao tu wana hatimiliki ya kufanya siasa katika kisiwa cha Pemba.

Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi Mkoa wa Kusini Pemba Abdalla Khamis alisema wamesikitishwa na tabia iliyojitokeza kwa wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi kushambuliwa wakati wanaporudi katika mikutano ya kisiasa.

“Tunawaomba wafuasi wa CCM wawe watulivu katika kipindi hichi cha kampeni za kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 28...dawa yao ipo ni kukipatia ushindi wa kishindo chama cha Mapinduzi''alisema Khamis.

Mapema daktari katika Hospitali ya Chake Chake Pemba Yahya Faki alisema majeruhi saba waliopokelewa katika hospitali hiyo hali zao zinaendelea vizuri na uchunguzi unaonesha walishambuliwa kwa kupigwa mawe na vitu vyenye ncha kali.

Hilo ni tukio la pili kwa wafuasi wa CCM kushambuliwa. Katika tukio la kwanza  viongozi na wafuasi wa CCM walivamiwa kwa kupigwa mapanga wakiwa katika nyumba ya ibada Kangagani Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Yusuph Masauni alilitaka Jeshi la Polisi kuchunguza haraka na kuwakamata wahusika na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.

MKURUGENZI Mkuu wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS), ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi