loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Maalim Seif amshambulia Membe

MWENYEKITI wa Chama cha ACT-Wazalendo Seif Sharrif Hamad, amesema chama hicho hakimtambui Bernard Membe kuwa ni mgombea wa urais wa Tanzania kupitia chama hicho.

Maalim Seif alisema jana kuwa, ACT Wazalendo walikubaliana kumuunga mkono mgombea wa urais kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu hivyo hawamtambui Membe kuwa ni mgombea wao.

Juzi Membe alisema, atafanya kampeni za kishindo ndani ya dakika za ‘lala salama’ kuwania urais kupitia chama hicho na atafanya maajabu.

Maalim Seif aliwaeleza waandishi wa habari kuwa, hawamtambui Membe kwa kuwa chama kilifanya vikao vikiwemo vya Halmashauri Kuu Taifa na Kamati Kuu vikaamua hivyo na kwamba, Membe alihudhuria.

Alidai kushangazwa na hatua hiyo ya Membe kujitangaza kuwania kiti hicho wakati hajafanya mikutano ya kampeni kunadi sera za chama hicho.

 

“Membe ni mtu aliyepo ndani ya chama chetu ambaye anaonekana kuwa na mapenzi na CCM, anaonekana ameletwa kwa sababu maalumu, msimamo wetu kama chama na nawatangazia wanachama wote kuachana naye na zaidi twende na Lissu” alisema.

Alisema kinachofanywa na Membe kwa sasa kujitangaza kuwa ni mgombea urais kupitia chama hicho ni sawa na kutaka kuwatoa katika  mstari ili wasifikie malengo yao na akadai kuwa huenda mwanasiasa huyo anatumika kuwavuruga.

“Mimi Mwenyekiti wa chama, Halmashauri Kuu pamoja na Kamati kuu, nasisitiza kuwa tulikaa kikao cha Membe akiwemo ndani na kutoa uamuzi juu ya suala hilo na kukubaliana kuwa tumpe Lissu kura za urais, inashangaza kumuona mwenzetu anakwenda kinyume na yale tuliyokubaliana na kujinadi kuwa yeye ni mgombea” alisema Maalim Seif

Alisema kupitia vikao na Membe akiwemo, walimweleza kuhusu azma yao kuhusu ulazima wa kushirikiana na vyama vingine siasa kwa lengo la kuchagiza ushindi naye alikubali uamuzi huo.

Maalim Seif alisema, suala hilo haina maana kuwa kuna mpasuko au mgogoro ndani ya chama hicho isipokuwa ni utaratibu ambao wao kama chama waliona vyema iwe hivyo kutokana na nguvu anayaoonekana kuwa nayo Lissu kukabiliana na mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) John Magufuli.

MKURUGENZI Mkuu wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS), ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi