loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Serikali yatoa msimamo riba mikopo kwenye kilimo

NAIBU Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema kuanzia sasa serikali haitaruhusu mkopo kutoka benki yoyote nchini kwenda sekta ya kilimo ambao riba yake itakuwa zaidi ya asimilia mbili.

Bashe alisema mifumo ya fedha za mikopo ambayo imekuwa ikitumiwa na benki kuwezesha sekta ya kilimo imepitwa na wakati kwa kuwa haina uhusiano na sekta hiyo na pia haiwezi kuendeleza wakulima.

Alitoa msimamo huo mjini Bariadi wakati wa kikao cha wadau wa zao la pamba Mkoa wa Simiyu.

Kikao hicho kilikuwa na lengo la kujadili taarifa ya utekelezaji mpango mkakati wa mageuzi ya zao la pamba kwenye mkoa huo.

"Kuanzia sasa hatutaki mkopo wowote wenye riba ya asimilia 18 au zaidi, mkopo ambao tunautaka usizidi riba asilimia mbili, anayetaka aje, asiyetaka hatutaki mkopo wake, tumeona inawezekana mkopo kuwa na riba ya asilimia mbili," alisema Bashe.

Alisema masharti ambayo yamekuwa yakiwekwa na benki kutoa mikopo katika kilimo yamekuwa magumu na kuonekana kutowasaidia wakulima, hivyo kusababisha benki nyingi kupeleka kiasi kidogo katika sekta hiyo.

Kwa mujibu wa Bashe serikali haitakuwa tayari kufanya kazi na benki kama itaendelea kutoza asilimia 18 na riba ya mikopo ya kuiwezesha sekta hiyo.

"Kwa sasa hatutaruhusu mifumo ya kizamani ambayo inamlazimu mkulima kuanza kufanya marejesho kabla hata ya kuzalisha, mfano kwenye zao la korosho linalochukua miaka miwili kuvuna...sasa kwa hali hiyo, mkulima anatoa wapi fedha za marejesho wakati hajavuna na kuingia sokoni,” alihoji.

Bashe alisema, msimu uliopita wa zao la pamba benki ya NMB ilitoa fedha za kununulia dawa za wadudu kwa riba ambayo haikuzidi asilimia mbili.

"Msimu uliopita NMB walitusaidia bilioni nane, lakini kwa sharti la riba ambayo haizidi asilimia mbili, na walifanya hivyo wakatoa mkopo wa bilioni 8, kama tungelitumia mifumo yao riba ailitakiwa kuwa asilimia 18 au zaidi," alisema.

Bashe alisema benki zizonataka kusaidia sekta ya kilimo nchini inayochangia asilimia 30 ya pato la taifa, lazima wabadilishe mifumo na kuona kilimo kama fursa muhimu katika kufanya biashara.

Katika kikao hicho, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antohny Mtaka alisema serikali imepeleka zaidi ya Sh bilioni 1.2 kulipa madeni ya wakulima wa pamba ikiwa ni awamu ya pili ya malipo hayo.

Alisema ndani ya wiki hii wakulima wote wa mkoa huo, watakuwa wamelipwa madeni waliyokuwa wanadai katika msimu uliopita wa zao hilo.

Mtaka aliwataka viongozi wa Amcos ambao wameanza kupokea malipo hayo, wahakikishe fedha zinawafikia wakulima kwa wakati na akawaonya kama watafanya tofauti na hivyo.

MKURUGENZI Mkuu wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS), ...

foto
Mwandishi: Happy Mollel, Simiyu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi